Umati wa
waumini wa dini ya Kiislam waliokwenda kuhiji Macca, Saudi Arabia.
|
Wakiwa
wamefunika midomo yao kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusambaa kwa njia
ya hewa.
Watu
walikuwa wakielekea eneo la kurushia mawe, na wengine wakitokea huko pale
ghafla watu walipoanza kuanguka.
Kulikuwa na
raia wa Nigeria, Niger, Chad na Senegal miongoni mwa mataifa mengine.
Idara ya
ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema mkanyagano huo ulitokea pale kulipotokea
"ongezeko la ghafla" la watu waliokuwa wakielekea kwenye kwenye nguzo
za kurushiwa mawe.
Waziri wa
afya wa Saudi Arabia Khaled al-Falih amesema mkanyagano huo ulitokea kwa sababu
mahujaji walikosa kufuata maagizo.
"Wengi
wa wahamiaji huenda bila kufuata ratiba iliyowekwa," amesema.
Mwandishi wa
BBC Hausa Tchima Illa Issoufou aliyekuwa ameenda kuhiji ni mmoja wa
walioathirika. Anasema shangazi yake alifariki na baadhi ya watu alioandamana
nao hawajulikani waliko.
"Watu walikuwa
tu wakiimba jina la Allah, huku wengine wakilia, wakiwemo watoto. Watu
walianguka sakafuni na hakukuwa na wa kuwasaidia. Ni kana kwamba kila mtu
alikuwa anajijali mwenyewe," amesema.
Mkanyagano
huo umetokea siku ya kwanza ya sherehe za Eid al-Adha.
Idara ya
ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema maafisa 4,000 wametumwa eneo hilo kusaidia
pamoja na wahudumu 200 wa huduma za dharura.
Waumini wa
dini ya Kiislam wakiwa katika swala maalumya hija,Macca, Saudi Arabia.
Maandalizi
ya ibada hizo za hija yalikuwa yamekumbwa na mkasa baada ya kreni kuanguka
katika msikiti mkuu wa Mecca mwezi huu na kuua watu 109.
Hii si mara
ya kwanza kwa mikasa kutokea wakati wa hija.
Mikasa
mingine iliyotokea wakati wa kuhiji:
2006:
Mahujaji 364 walifariki wakati wa kurushia mawe mnara unaoashiria shetani
1997:
Mahujaji 343 walifariki na 1,500 kujeruhiwa kwenye mkasa wa moto
1994: 270
waliuawa katika mkanyagano
1990:
Mahujaji 1,426 waliuawa katika mkanyagano njia za kupitia chini za kuelekea
maeneo matakatifu
1987: Watu
400 walifariki maafisa wa serikali walipokabiliana na waandamanaji waliounga
mkono Iran.Source...BBC Swahili.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment