Baadhi ya
Watanzania walioko Hijja na ambao wamenusurika na maafa ya msongamano wa watu
huko Mina jana. Kulia nia Bw. Yahaya Sameja, kushoto ni mwigizaji mchekeshaji
Bw. Amri Athumani al maarufu kama King Majuto. Wa katikati jina lake halikuweza kupatikana.
------------------------------------------------------------------------------------
Bismilah
Rahman Raheem
Assalaam
alaykum warahmatullahi wa barakaatuhu.
Taarifa hii
inahusu tukio lilitokea jana Mina Saudi Arabia wakati
mahujaji wakielekea kwenye Jamaraat , palitokea msongamano mkubwa ( stampede) na
kupelekea mahujaji zaidi ya 700 kufariki na mamia kadhaa kujeruhiwa.
Tayari
tumethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokea Tanzania
miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine
wanne ni Watanzania.
Watanzania
waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni Bi Mwanaisha
Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla.
Mwanamke
mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikana hadi
Alhamisi usiku wakati tukiandaa taarifa hii.
Raia wa
Kenya ametambuliwa kwa jina la Bi Fatuma Mohammed Jama.
Kuna taarifa
ya mahujaji wanawake wawili ambao hadi Alhamisi usiku
walikua hawajapatikana hivyo hatukua na uhakika juu ya usalama wao hadi tutakapowaona
ama kupata taarifa zao.
Ifahamike kuwa majina yamepatikana kupitia vitambulisho
vyao ambavyo
wahanga wa tukio hili waliweza kuvichukua kutoka kwenye miili ya marehemu.
Nimepokea
taarifa za majeruhi miongoni mwa mahujaji wetu wa Tanzania na
baadhi ya majeruhi hao nimeonana nao mara baada ya kuruhusiwa kutoka
hospitalini.
Vilevile
nimeagiza maafisa wetu wa Bakwata nilionao hapa Mina kuendelea
kufuatilia habari na taarifa za mahujaji wetu katika hospitali na sehemu za
kuhifadhia maiti.
Nimefanya hivyo ili niweze kuwa na uhakika juu ya usalama wa mahujaji
wetu.
Katika
kipindi hiki cha taharuki kubwa tunafanya mawasiliano na wizara
husika hapa Saudi Arabia kwa kushirikiana na serikali yetu kupitia ubalozi wetu
hapa Saudi Arabia.
Natambua uwepo wa mkanganyiko wa taarifa ambazo zinazidisha taharuki kwa
ndugu na jamaa wa mahujaji wetu.
Nachukua fursa hii kuwaomba ndugu na jamaa wa
mahujaji kuwa watulivu na
kuwa na subra katika wakati huu mgumu sana kwetu sote.
Tunaendelea
kufuatilia kwa karibu sana na Insha Allah mara tu tukipata
taarifa za uhakika basi tutawafahamisha.
Kutokana na
idadi ya maiti kuwa kubwa serikali ya Saudi Arabia wanaendelea
na zoezi la kutambua uraia wa kila mwili ili waweze kutoa taarifa tunatarajia
wakati wowote tutakuwa tumepata taarifa zaidi.
Wabillahi
Tawfiiq.
Sheikh Abu
Bakari Zuberi
Mufti wa
Tanzania.
MECCA, Saudi
Arabia.
|
No comments:
Post a Comment