Umoja Wa
Vyama vinavyounda UKAWA hapo Jana September 24,2015, wamezungumza na waandishi wa habari kwenye makao
yao makuu yaliyopo maeneo ya Kawe,jijini Dar kuhusu utafiti uliofanywa hivi
karibuni na taasisi ya TWAWEZA kuhusu mwenendo wa uchaguzi mkuu hapa nchini.
Akizungumza
kwa niaba ya UKAWA,Mwenyekiti Wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia alisema kuwa taarifa
ya taasisi hiyo imeidhalilisha TWAWEZA wenyewe na CCM kwa ujumla.
"TWAWEZA
imejidhalilisha kwa kubagua wagombea urais Wa vyama vingine mbali na CCM na
CHADEMA"
"TWAWEZA
haifahamu hata idadi ya wagombea ubunge na udiwani,utafiti huo umetoa ripoti
inayokinzana na ukurasa wa saba,huu utafiti ni Wa uongo" alisema Mbatia.
"Katika
taarifa ya TWAWEZA haijaweza kuhakiki taarifa yake kitakwimu,CCM imekubaliana
na idadi ya watu walioshiriki kwenye utafiti kwa kigezo cha idadi ya watu
1848"
"CCM
hiyo hiyo ilikataa kukubali maoni ya wananchi zaidi ya laki tatu kwenye rasimu
ya katiba ya Warioba,lakini leo wamekubali watu 1848" aliongeza Mbatia.
"Simu
za mkononi na chaja zilizogawiwa ilikuwa ni rushwa iliyotolewa na TWAWEZA kwa
washiriki Wa utafiti huo"
"TWAWEZA
wanajua vyama vya CUF,NCCR-MAGEUZI,na NLD hawajatoa wagombea wao Wa urais
isipokuwa CHADEMA ila wameweka swali hilo,kwakuwa TWAWEZA ni taasis
inayothamini midahalo tunawaalika kwenye midahalo ya kutetea taarifa ya utafiti
wao".
Akizungumzia
kuhusu UKAWA kupata mwaliko Wa kufanya mdahalo Wa mgombea wao Wa urais alisema
kuwa hakuna taasis yoyote iliyoleta barua kwa mgombea urais,Edward Lowassa
kushiriki kwenye midahalo.
"Utafiti
wa ndani Wa UKAWA uliofanywa na watafiti guru kutoka nje ya nchi ulionyesha
Edward Lowassa atapata kura 74%".alisema Mbatia.
Naye
Prof.Baregu alisema kuwa sampuli ya data za utafiti Wa TWAWEZA imechafuliwa kwa
makusudi ili kupotosha umma.
"Mtafiti
kutoka Oxford University niliongea naye aliona kuwa UKAWA inaweza kushinda ila
siyo kwa gap kubwa"alisema Baregu.
HAPA CHINI BONYEZA KUSIKILIZA VIDEO YA MKUTANO HUO
|
No comments:
Post a Comment