LA LIGA 2015 / 2016 :- Ronaldo kufunga Bao 5 mguuni kwake wakati Real Madrid inaichapa RCD Espanyol Bao 6-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 12, 2015

LA LIGA 2015 / 2016 :- Ronaldo kufunga Bao 5 mguuni kwake wakati Real Madrid inaichapa RCD Espanyol Bao 6-0.

Baada ya kutofunga katika Mechi 2 za kwanza za Msimu mpya wa La Liga, Leo hii September 12,2015, huko Estadi Cornella-El Prat Jijini Barcelona, Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo alilipuka na kupiga Bao 5 mguuni kwake wakati Real Madrid inaichapa RCD Espanyol Bao 6-0.

 Bao hizo zimemfanya awe ndio Mfungaji Bora katika Mechi za La Liga katika Historia ya Real Madrid kwa kumpiku Raul mwenye Bao 228 na sasa yeye ana Bao 230.
Leo September 12,2015, Ronaldo alianza kwa kupiga Hetitriki ya ndani ya Dakika 13, ikiwa ni Hetitriki yake ya 29 kwenye La Liga akiendelea kushika Rekodi hiyo, kwa Bao za Dakika za 7, 17 na 20.

Karim Benzema ndie alieifungia Real Bao la 4 na Ronaldo kuongeza tena Bao 2 katika Dakika za 61 na 81.
Hii ni mara ya pili kwa Ronaldo kufunga Bao 5 katika Mechi baada ya Aprili 5 Mwaka huu pia kupiga 5 wakati Real ikiifunga Granada 9-1.

LA LIGA 2015 / 2016 RATIBA/MATOKEO

Ijumaa Septemba 11,2015.

Levante 1 – 1 Sevilla FC 

Jumamosi Septemba 12,2015.

RCD Espanyol 0  - 6 Real Madrid CF

1915 Sporting Gijon v Valencia C.F

2130 Atletico de Madrid v FC Barcelona

2300 Real Betis v Real Sociedad

Jumapili Septemba 13,2015.

1300 Granada CF v Villarreal CF

1700 Athletic de Bilbao v Getafe CF

1915 Celta de Vigo v Las Palmas

2130 Malaga CF v SD Eibar

Jumatatu Septemba 14,2015.

2130 Rayo Vallecano v Deportivo La Coruna

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.       

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad