UCHAGUZI MKUU 2015:- Kazi ya NEC imefikia hapa mpaka sasa hivi.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 13, 2015

UCHAGUZI MKUU 2015:- Kazi ya NEC imefikia hapa mpaka sasa hivi..

Vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vilivyowasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.

October 25 2015 Watanzania watashiriki Uchaguzi mkuu wa Kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani.

 Wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Uchaguzi huu 2015 ni pamoja na Dk. Magufuli wa CCM na Lowassa wa Chadema anayewakilisha pia muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF), wanachuana pia na Fahmy Dovutwa wa UPDP, Hashim Rungwe wa Chama cha Umma (Chauma), Maximillian Lymo wa TLP, Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, Chief Lutasola Yemba wa ADC na Janken Kasambala wa NRA.

Kwa hisani ya  MICHUZI BLOG, Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, Frolence Turuka ametembelea Ofisi za NEC na kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu yalipofikia.

Tayari vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vimepokelewa katika Ofisi ya NEC na maandalizi yamefikia hatua nzuri kabisa mpaka sasahivi.
Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka akimpatia maelekezo juu ya NEC inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo alipoitembelea kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimuonyesha Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka moja ya vifaa vilivyowasili kwa ajili ya kusaidia Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad