 |
Toka tarehe
29 August 2015 ulipofanyika uzinduzi wa kampeni Ukawa bado wameendelea kusogea
sehemu mbali mbali za kuwafikia wananchi na leo Sept 10,20145 Mkoani Dodoma
katika wilaya ya Kongwa mji mdogo Kibaigwa katika uwanja wa Amani wamefanya
mkutano na Edward Ngoyai Lowassa na amewataka watanzania kuiwezesha UKAWA
kuingia madarakani ili waanze kazi ya kuondoa kero za wananchi zilizoshikana
chini ya utawala wa CCM kutokana mfumo kandamizi zikipata ufumbuzi kwa muda
mfupi likiwemo tatizo la maji.
Tatizo la
maji ni miongoni mwa yanayolalamikiwa kwa muda mrefu na asilimia kubwa ya watanzania
wakiwemo wa mikoa ya kanda ya kati ambalo, wananchi hawa wa Gairo ambao ni
sehemu kidogo ya watanzania wanaolalamikia wanathibitisha.
Tatizo la
udhaifu wa katiba na usimamizi wa sheria ni miongoni mwa mambo yanayoelezwa na
viongozi waandamizi wa UKAWA akiwemo Mh Tundu Lisu kuchangia umasikini
unaowakabili wananchi.
Mh Lowassa
bado anaendelea kunadi sera za UKAWA katika majimbo mbalimbali ya mkoa wa
Dodoma kabla ya kuhamia mikoa ya Singida na Shinyanga na hapa kukusogezea kila
kinachonifikia na hapa nimekuwekea picha za mkutano mtu wangu...Picha kwa Hisani ya Millardayo/ na itv.
|
 |
Wakazi wa
Kibaigwa wakiwa karibu na usafiri wa mgombea uraisi 2015.
|
 |
Frederick
Sumaye akizungumza na wakazi wa Kibaigwa.
|
 |
Wengine
walifanya maamuzi ya kukaa chini
|
 |
Hili ndio
gari lililokuwa likitumika kama jukwaa.
|
 |
Hawa ndio
wagombea kwa nafasi ya udiwani wakitambulishwa na mgombea urais Edward Lowassa
|

Edward Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kongwa Essau Ngobei
 |
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |
No comments:
Post a Comment