Mashuhuda
waliobaini kuwepo kwa tukio hilo
wamesema inawezekana linatokana na imani
za kishirikina.
Wamesema
walifika katika makaburi hayo kwa ajili ya kumsitiri ndugu yao aliyefariki
lakini cha kushangaza wakaona juu ya moja ya makaburi kukiwa na vitu hivyo na
kudai kuwa huenda marehemu alizikwa navyo.
"Sisi
tulikuwa na msiba wetu..tukaja hapa makaburini kumzika ndugu yetu, ghafla
tukaona juu ya kaburi jingine kuna vitu hivyo..inaonekana huyu marehemu
alizikwa na vitu vyake vikaletwa hapa makaburini na kuwekwa juu ya kaburi
lake",ameeleza mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Stanslaus
Rweyemamu.
Kufuatia
taarifa hizo waandishi wa habari bila kupoteza muda
walifika katika eneo la tukio na kukuta vitu hivyo vikiwa juu ya kaburi la
marehemu, huku wahusika waliofanya hivyo wakiwa hawajulikani kutokana na
wahusika wa msiba kutokujulikana.
Hata hivyo
baada ya askari polisi kufika eneo la tukio walivichukua vitu hivyo na kuondoka
navyo kituo cha polisi Bariadi .
Kamanda wa
polisi Mkoani Simiyu Gemini Mushy
amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na
kwamba wanaendeela kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo. |
No comments:
Post a Comment