KOMBE LA DUNIA WANAWAKE 2015:-Taswira Picha wakati Marekani walivyosheherekea kutwaa ubingwa huo usiku wa leo Julai 06,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 06, 2015

KOMBE LA DUNIA WANAWAKE 2015:-Taswira Picha wakati Marekani walivyosheherekea kutwaa ubingwa huo usiku wa leo Julai 06,2015.

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Marekani ( USA ) imetwaa Kombe la Dunia kwa Kinamama baada ya kuwacharaza Japan Bao 5-2 kwenye Fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo Julai 06,2015 huko BC Place Nchini Canada.

Shujaa wa Mechi hii kwa Marekani ni Kepteni wao Carli Lloyd ambae alipiga Hetitriki ndani ya Dakika 16 wakati USA ikiongoza Bao 4-0 katika Dakika hizo 16 za mwanzo.

Mara baada ya Mpira kwisha Rais wa CAF, Issa Haytou, aliemwakilisha Rais wa FIFA Sepp Blatter, alikabidhi Kombe la Dunia kwa USA.

Hii ni mara ya 3 kwa USA kutwaa Kombe la Dunia kwa Kinamama na kisasi kwa kutolewa na Japan kwa Penati kwenye Fainali ya 2011 iliyoisha Sare ya 2-2.





Carli Lloyd  na tuzo yake ya mchezaji bora katika fainali hizo, akifunga magoli katika  Dakika ya 3, 5 na 16,Lauren Holiday 14,Tobin Heath 54 huku ya Japan yakifungwa na Yuki Nagasato Dakika ya 27,Julie Johnston 52 [Kajifunga mwenyewe]

Juzi, England ilitwaa Nafasi ya 3 katika Kombe la Dunia baada ya kuibwaga Germany 1-0 kwa Goli la Dakika za Nyongeza 30.

Bao la 3 la Carli Lloyd lilifungwa toka Mstari wa Kati baada ya Staa huyo kumwona Kipa wa Japan Ayumi Kaihori akiwa ametoka Golini na kupiga Mpira wa juu ambao Kipa huo aliuparaza kwa Vidole vyake lakini ukagonga Posti na kutinga.




Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad