Askari
wakiimarisha ulinzi wakati wa uchaguzi wa wabunge nchini Burundi.
Viongozi hao
wakiwemo Mwenyekiti na Mwenyeji wa Jumuiya, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na
Yoweri Museveni wa Uganda, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta walipendekeza uchaguzi
uahirishwe kufuatia mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.
Shinikizo
hilo la kuahirisha uchaguzi lilitokana na Umoja wa Afrika, na Umoja wa Mataifa,
jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki, pamoja na kikosi cha kimataifa kuhusu eneo la
maziwa makuu.
Umoja wa
Mataifa umesema kwamba, idadi kubwa ya watu waliokimbia walisema nchi hiyo
inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kisiasa.
Zaidi ya
raia laki moja wa Burundi wamekimbia nchi hiyo tangu mwezi Aprili,2015,wakati
kulizuka ghasia kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Hii ilikuwa
ni mara ya tatu kwa uchaguzi huo kuahirishwa baada ya tume ya uchaguzi
kuahirisha uchaguzi kwa majuma matatu kutokea Juni 26 hadi Julai 15 mwaka huu
na sasa kusogezwa tena mbele hadi Julai 21 mwaka huu.
Source:-Na BBC
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Sunday, July 12, 2015
BURUNDI:-Uchaguzi waahirishwa tena Mpaka Tarehe hii 2015.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment