Awali Neymar
alianza kuonesha vitendo ambavyo si vya kiungwana kwenye soka pale alipojaribu
kufunga goli kwa kutumia mkono lakini baadae ‘akambabua’ na mpira Pablo Armero
na kutaka kumpiga kichwa Jeison Murillo.
Kukosekana
kwa Neymar kutamfanya kocha wa Brazil Carlos Dunga amtumie Robinho kama mbadala
wa Neymar kwenye mechi ijayo dhidi ya Venezuela.
Dunga
amekuwa akiwatumia Robinho na Douglas Costa kwenye mazoezi ili kujaribu
kutengeneza uwiano mzuri kati yao wakati pia kiungo wa Liverpool Philipe
Coutinho anatarajiwa kuanza kwenye mchezo huo ambao utakuwa ni wa kwanza kwake
tangu kuanza kwa mashindano.
Robinho
amejumuishwa kwenye kikosi cha Dunga mwaka jana baada ya kuikosa michuano ya
kombe la dunia wakati huo kocha akiwa Scolari. Robinho ambaye alishawahi
kukipiga Real Madrid, Manchester City na AC Milan kwasasa anacheza kwenye klabu
ya Santos ya Brazil.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment