COPA AMERICA:- Taswira Picha wakati Argentina,Paraguay,Uruguay zikitinga Robo Fainali Leo June 21, 2015 ni Brazil.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 21, 2015

COPA AMERICA:- Taswira Picha wakati Argentina,Paraguay,Uruguay zikitinga Robo Fainali Leo June 21, 2015 ni Brazil..


Chile imetoa kipondo cha mbwa mwizi kwa Bolivia baada ya kuichakaza kwa jumla ya bao 5-0 ikiwa ni mchezo wa kundi A kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya bara la America Kusini  almaarufu kama Copa America mchezo uliomalizika alfajiri ya leo June 21, 2015 huko nchini Chile.

 Charles Aranguiz alianza kuipatia Chile bao la mapema ikiwa ni dakika ya tatu tangu mchezo huo kuanza kabla ya winga wa Arsenal Alexis Sanchez kufunga goli la pili dakika ya 37 na kuifanya Chile iende mapumziko ikiwa mbele kwa goli 2-0 dhidi ya Bolivia.

Aranguiz alipachika pao la tatu kwa Chile dakika ya 66 lakini likiwa ni bao lake la pili kwenye mchezo huo, kabla Gary Medel hajatupia nyavuni goli la nne dakika ya 80. 

Zikiwa zimebaki dakika nne ili mwamuzi amalize pambano hilo, Raldes wa Bolivia alijifunga na kuufanya mchezao huo kumalizika kwa wenyeji wa mashindano (Chile) kuibuka na ushindi mnono wa goli 5-0 na Chile sasa kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali kwenye michuanon hiyo.

Kwenye mchezo wa awali uliozikutanisha Mexico dhidi ya Ecuador kwenye mchezo wa kundi A, timu ya Mexico imetupwa nje ya mashindano ya Copa America baada ya kukubali kichapo cha goli 2 -1 kutoka kwa Ecuador kwenye mechi ya mwisho ya timu za kundi A.

Miller Bolanos alianza kuipatia Ecuador bao la kuongoza dakika ya 26 kabla ya mshambuliaji wa West Ham Enner Valencia kuongeza goli la pili dakika ya 57 kwa upande wa Ecuador. 

Mexico walipata goli lao la kufutia machozi dakika ya 64 kwa mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Raul Jimenez.

Higuain amefunga goli pekee lililoipeleka Argentina kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America inayozidi kushika kasi huko Chile. 

Goli la Argentina limefungwa mapema kipindi cha kwanza dakika ya 11, goli hilo liliipa Argentna ushindi wa goli 1-0 mbele ya Jamaica ‘Reggae boys’ ambao hawajashinda mchezo wowote kwenye kundi B.

Ushindi huo unaifanya Argentina kumaliza ikiwa kinara wa kundi B na huenda ikakutana na Ecuador, Peru au Venezuela kwenye mtanange wa robo fainali utakaopigwa siku ya Ijumaa.

Nyota wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi alicheza mechi yake ya 100 akiwa ndani ya uzi wa Argentina akiisaidia timu yake kufuzu na kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali. 

Messi ambaye mpaka sasa bado hajatwaa taji lolote akiwa na timu yake ya taifa licha ya mafanikio makubwa aliyopata kwenye ngazi ya klabu, mafanikio makubwa aliyopata akiwa na timu ya taifa ni kuifikisha timu hiyo kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka jana dhidi ya Ujerumani lakini timu yake iliambulia kichapo na kombe hilo likaenda Ujerumani.

Mchezo wa kwanza wa kundi B uliikutanisha Uruguay dhidi ya Paraguay ambapo pambano hilo lilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya kufungana goli 1-1 lakini Uruguay wamekata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo.

Jose Gimenez alianza kuifungia Uruguay goli la kuongoza dakika ya 29 ya mchezo lakini Lucas Barrios aliisawazishia Paraguay goli hilo japo sare hiyo haijawasaidia Paraguay kusonga mbele kwenye mashindano hayo makubwa kwa bara la Amerika ya Kusini.

MSIMAMO.

KUNDI A


**Kila Timu imecheza Mechi 3

1 Chile Pointi 7
2 Bolivia 4
3 Ecuador 3
4 Mexico 2

KUNDI B

**Kila Timu imecheza Mechi 3

1 Argentina Pointi 7
2 Paraguay 5
3 Uruguay 4
4 Jamaica 0

KUNDI C

**Kila Timu imecheza Mechi 2 

1 Peru Pointi 3
2 Brazil 3
3 Colombia 3
4 Venezuela 3 

**Timu 2 za Juu kila Kundi na Timu za 3 mbili Bora zitasonga Robo Fainali

++++++++++++++++++++++

Kwenye Robo Fainali Mabingwa Uruguay watacheza na Wenyeji Chile, Argentina watacheza na Mshindi wa 3 toka Kundi C na Paraguay watacheza na Bolivia.

Leo zipo Mechi mbili za mwisho za Kundi C ambalo Timu zozote 3 kati ya 4 zinaweza kutinga Robo Fainali kwa vile zote zina Pointi 3 kila mmoja.

Brazil watacheza na Venezuela na Peru kuivaa Colombia.


COPA AMERICA NUSU FAINALI


Jumatatu Juni 29,2015.

RF1 v RF2 (Saa 8 na Nusu Usiku)


Jumanne Juni 30,2015.

RF3 v RF4 (Saa 8 na Nusu Usiku)

MSHINDI WA 3

Ijumaa Julai 3,2015.

(Saa 8 na Nusu Usiku)

FAINALI

Jumamosi Julai 4,2015.

(Saa 5 Usiku)

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad