UHAI NA MAFANIKIO:-Fahamu Rekodi iliyofikiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana katika ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 29, 2015

UHAI NA MAFANIKIO:-Fahamu Rekodi iliyofikiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana katika ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mkutano huo umefanyika kwenye viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini Mwanza jioni ya Jana June 28, 2015. 

Ndugu Kinana ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, tayari wamesafiri umbali wa Km 193,537, kwa kufika katika Wilaya 163, majimbo 239, nusu ya vijiji na kata 1938 za Tanzania. Pia msafara wake ulitumia jumla ya saa 84 kuzunguka mikoa yote hiyo, na kusafiri kwa mitumbwi katika visiwa 16. Amehutubia jumla ya mikutano ya ndani/hadhara 1918 na kujikusanyia wanachama wapya 284,300 ambapo kutoka upinzani 38,984.

Katibu  Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (Pichani ) ameahidi kuwa watafanya mageuzi ambayo yanaifanya Halmashauri Kuu ya Chama (NEC) hicho kuwa na nguvu katika kuisimamia serikali yake.

Akihutubia jana June 28, 2015, mjini Mwanza, alisema hiyo ni kuongeza uwajibikaji wa viongozi na watumishi ndani ya Serikali ili vyeo walivyo navyo viwe vya utumishi na sio vya utukufu ili kuongeza ufanisi ndani ya Serikali.

Alisema watu wakishapata vyeo na madaraka wanajisahau na vyeo vinageuka vyao na si vya wananchi. Alisema umezuka ugonjwa wa ‘mheshimiwa’ kwa maana mtu akishapata cheo hata kama alikuwa kwenye jamii, anajiita mheshimiwa.

“Mtu alikuwa mbunge, rais anamuita anampa uwaziri, anakuwa zaidi ya wananchi.” Alisema watu wanageuza vyeo kuwa vya utukufu. Alisema kila mkoa aliopita, aliuliza ni mara ngapi mawaziri wamepita kusikiliza wananchi, ni wachache.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiagana na wananchi mara baada ya kumaliza kuwahutubia kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jioni ya jana June 28,2015,Kinana aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa bunge lijalo kwa upande wa CCM, litakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali kuhusu utendaji wake.

Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita, Twalib Ngika, akikabidhi kadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza Jana June 28,2015..


Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akihutubia kwenye mkutano huo.

Katibu mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nanuye akiwapungia mkono wananchi alipokuwa wakiwasili kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, ambapo aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa bunge lijalo kwa upande wa CCM, litakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali kuhusu utendaji wake.

 “Ngoja niwaahidi kuwa ndani ya chama hiki tutajitahidi kuleta mbadiliko makubwa, vikao vya chama viwe na nguvu kuisimamia serikali yake, kwani sasa hivi tunabembeleza,” alisema Kinana Alisema chama lazima kiwe na nguvu kuliko serikali kuliko ilivyo sasa chama kinaibembeleza Serikali, hatuwezi kuwa na katibu wa CCM ambaye hawezi kuhoji mawaziri.

Alisema wabunge wa CCM wawe na nguvu ya kuikataa miswada ya Serikali kama miswada hiyo ni ya ovyo ambayo haijali maslahi ya wananchi. “Eneo la kufanyia kazi ni kamati ya wabunge wa CCM tutafanya mageuzi kwenye kamati hiyo.

Lazima tubadilishe mfumo wa kamati ya chama bungeni. Mambo ya wabunge wa CCM kuunga mkono kila kinacholetwa serikalini,” alisema.

Alisema mara baada ya uchaguzi kikao chake cha kwanza baada ya kuchaguliwa, ni kukutana na wabunge wa CCM. “ Jambo la ovyo likiletwa bungeni na serikali walikatae,” alisema Kinana na kuongeza, “Kwa hiyo tutakaa na wabunge wangu tutatengeneza muundo mpya kwamba waziri mkuu ndiyo kiongozi wa wana CCM bungeni.

“Nataka nipendekeze sheria zinazogusa maisha ya watu na baadaye zinakuwa kero, zifutwe haraka sana bungeni. Wananchi wawe wanaulizwa kuhusu sheria zinazotungwa,” alisema.

Pia alisema hawawezi kuwa na kiongozi wa Serikali bungeni halafu huyo huyo anakuwa kiongozi wa wabunge wa chama hicho au katibu wa wabunge wa CCM halafu anakuwa ni waziri.



Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CCM kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Jana June 28, 2015.


Malikia wa taarab, Khadija Kopa akiongoza kuimba wimbo maalum wa CCM, wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Furahiha jijini Mwanza.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad