Kikosi Kazi Ngoma Africa band
Mining City,Austria.
Bendi maarufu ya muziki wa dansi
barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni,yenye makao nchini
Ujerumani,inatarijiwa kutumbuiza katika maonyesho makubwa ya muziki na
utamaduni Mamling Festival siku ya jumapili alhasiri katika viwanja vya
Schlosspark,Mamling 3, Mining nchini Austria.
watayarishaji wa onyesho hilo
wameitaja bendi hiyo ya Ngoma Africa band kuwa muziki wake ni sawa na mzimu
unawapeleka puta washabiki katika maonyesho ya kimataifa na washabiki nchini
Austria wanameisubiria kwa muda wa mwaka mzima.
Kikosi kazi hiko chenye tabia
ya kuwatia kiwewe washabiki wake kila waendako na kujizolea washabiki lukuki
kote duniani,kinaupeleka muzimu wa Bongo Dansi nchini Austria .Ziara ya bendi
hiyo imeingiliana na mwezi wa Ramadhani wakati baadhi ya wanamuziki wapo katika
swaumu lakini watatekeleza wajibu wao.
Ngoma Africa band iliyoanzishwa
mwaka 1993 na kiongozi wake Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja ni
bendi iliyobatizwa majina mengi ya kiusanii kutoka kwa washabiki majina kama
FFU-Ughaibuni, "Watoto wa Mbwa",Viumbe wa ajabu "Anunnaki Alien'
na mengi mengineyo.
Ni bendi yenye utajiri ya wanamuziki waliojaa vipaji, na
kwa sasa inatamba na nyimbo zake mbili mpyakatika CD " La Mgambo"
za kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda .
Sikiliza at
wasiliana nao at ngoma4u@gmail.com
|
Ngoma Africa
Band on action.
|
Ngoma Africa
Band at Oversea Museum in Bremen,German.
|
ngoma-africa_wordpress-36
Tubingen Festival 2014.
|
No comments:
Post a Comment