Waziri Mkuu
Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa,
akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma waliokuwa
wamesimama nje ya Ofisi za CCM Mkoa huo, mjini Songea jana Juni 21, 2015,
wakati alipofika kwa ajili ya kupata udhamini utakaomuwezesha kupata ridhaa ya
Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba
25, 2015.
WAZIRI Mkuu
Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina lake katika
vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama chao kitatenda haki
kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.
Lowassa
ameyasema hayo jana June 21, 2015 wakati akizungumza na wanachama wa CCM na
wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa
shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.
"Nimekuwa
mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya
CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya
utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi?
anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa
hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu". alisema Lowassa.
Lowassa
aliwasili Mkoani Ruvuma mapema mchana wa jana akitokea Mkoani Iringa kwa ajili ya
kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi ya chama hicho,
ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea kufunga barabara kuu ya
mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya kibambaza cha jengo la ofisi
ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza hao.
|
No comments:
Post a Comment