Wakati vikao vya uteuzi wa kada atakayepeperusha
bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika nafasi ya urais 2015 vikitarajia kuanza
wiki ijayo mjini Dodoma, imebainika kuwa mikoa ya Kanda ya Ziwa imeongoza kwa
kuwa na makada wengi waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama
hicho.
Uchunguzi
uliofanywa na NIPASHE umebaini kuwa mikoa hiyo ambayo ni Mwanza, Geita, Kagera,
Mara, Simiyu na Shinyanga ina makada tisa wa CCM waliochukua fomu kuomba
kuteuliwa na chama chao kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015.
Makada
hao ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira, Mbunge wa Afrika
Mashariki, Charles Makongoro Nyerere, Mbunge wa Kuteuliwa, Prof. Sospeter
Muhongo (Mara) Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (Geita), Waziri wa Uvuvi na
Maendeleo ya Mifugo, Dk. Titus Kamani (Simiyu), Balozi wa Urusi, Patrick
Chokala, Mbunge wa Sengerema , William Ngeleja , Luhaga Mpina (Mwanza), na mtoto wa marehemu
Jaji Francis Nyalali, Peter Nyalali (Kagera).
Mikoa ya
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ina wagombea saba na Kanda ya Kaskazini inafuatia
kwa kuwa na wagombea sita waliojitosa
katika kinyang’anyiro hicho.
Makada wa
CCM waliojitokeza katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ni Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof Mark Mwandosya, Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, na Musa Mwapango
(Mbeya), Mkurugenzi Mstaafu wa Usalama wa Taifa, Hassy Kitine, Dk. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wa Fedha mstaafu,
Monica Mbega (Iringa).
Kanda ya
Kaskazini makada wa CCM waliojitosa kuwania urais ni Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye (Arusha), Waziri wa
Katiba na Sheria Dk. Asha Rose Migiro , Dk.Muzzamil Kalokola, Litha Ngowi na Hellen Elinawinga
(Kilimanjaro), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January
Makamba (Tanga).
Kanda ya
Kati inafuatia ikiwa na wagombea watano ambao ni Waziri wa Uchukuzi, Samuel
Sitta, Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangallah (Tabora), Waziri wa Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (Singida),
na Dk. Mwele Malecela (Dodoma).
Wagombea
kutoka visiwa vya Zanzibar ni Balozi Amina Salum Ali, Makamu wa Rais,
Dk.Mohamed Gharib Bilal, Balozi Ali Karume na Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustine
Ramadhani.
Aidha, Kanda ya Kusini ina makada wawili ambao ni Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mathias Chikawe (Lindi).
Kanda ya
Magharibi imekuwa ya mwisho kutokana na kuwa na kada mmoja aliyechukua fomu
ambaye ni mkulima Lidephonce Bilohe (Kigoma).
Hata hivyo,
wapo makada wengine waliojitokeza ambao ni Amos Siyatemi, Samwel John, Leonce
Mulenda, Boniface Ndengo, Maliki Marupu
na Veronica Kazimoto.
Hadi kufikia
jana June 26,2015, takwimu zinanyesha makada 40
wameomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti hicho, Vikao vya CCM vitaanza Julai 5,
mwaka huu mjini Dodoma na Julai 11,2015 kutafanyika mkutano mkuu kwa ajili ya
kuchagua kada mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais.
Kanda ya
Mashariki ya Pwani inahusisha mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Mkoa wa Pwani
ambapo hadi sasa hakuna aliyejitokeza.
ZANZIBAR
Kwa upande
wa Zanzibar hadi sasa, makada wa CCM wanaoiomba nafasi hiyo ni Makamu wa Rais,
Dk. Mohamed Gharib Bilal, Balozi Amina Salum Ali, Balozi Ali Karume na Jaji
Mkuu mstaafu Augustine Ramadhani.
Makanda wengine waliojitokeza kuwania nafasi
hiyo ni Amos Robert Siyatemi, Musa Mwapango, Peter Isaiah Nyalali, Leonce
Nicholas Mulenda, Boniface Thomas Ndengo na Lidephonce Bilohe.
Chanzo:-
NIPASHE
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Saturday, June 27, 2015
Home
SIASA
RIDHAA URAIS CCM 2015:- Fahamu Kanda ipi inafata baada ya Kanda ya Ziwa kuongoza makada Urais.
RIDHAA URAIS CCM 2015:- Fahamu Kanda ipi inafata baada ya Kanda ya Ziwa kuongoza makada Urais.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment