Spika wa
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Pandu
Ameir Kificho alipokuwa akimkaribisha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
kuzungumza na wajumbe wa Baraza hilo pamoja na kulifunga rasmi Baraza
la nane la Wawakilishi katika ukumbi wa
Baraza Chukwani jana,June 26, 2015.Picha kwa Hisani ya FULL SHANGWE.
|
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Baraza la nane
la Wawakili wa Zanzibar jana,huko Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja.
|
Rais wa
Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein jana June 26,2015 ameufunga rasmi mkutano wa nane wa baraza
la wawakilishi huku kukiwa hakuna hata wajumbe na mawaziri kutoka chama cha
wananchi CUF, waliosusia vikao vya baraza hilo.
Akiwahutubia
wajumbe wa baraza hilo kutoka CCM na wageni waalikwa huko Chukwani, nje kidogo
ya mji wa Zanzibar, alisema kila mmoja anaelewa kwamba Baraza hilo linaendeshwa
kwa misingi ya Sheria na Kanuni.
Alisema
wakati Wajumbe wa Baraza hilo kutoka chama cha CUF waliposusia kikao cha baraza
hilo mwanzoni mwa wiki hii, hoja walizozitoa ambazo hawakuridhishwa na
uwandikishaji wa daftari la wapiga kura wapya, hazikuwa na mnasaba na hoja
iliyokuwa imewasilishwa ndani ya baraza hilo ili ijadiliwe.
“Siku hiyo
Waziri wa Fedha alikuwa amewasilisha hoja ya kujadiliwa kwa Muswada wa Sheria
ya Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambao haukuwa na uhusiano
hata kidogo na masuala ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga
kura,” alisema Dk Shein.
Alisema kuwa
hoja ya wajumbe hao wa CUF inahusiana na Sheria nyingine, ambayo ni Sheria ya
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, namba 9 ya mwaka 1992 inayosimamiwa na Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Sheria ya Usajili wa Mzanzibari Mkaazi, namba 7
ya mwaka 2005.
Aidha
alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuhakikisha kila mwananchi
mwenye sifa ya kupiga kura anapewa haki yake na kuwataka wanasiasa
wasiwapotoshe wananchi juu ya haki yao hiyo.
AMANI NA
USALAMA
Dk. Shein akizungumzia
hali ya amani na usalama alisema, siri kubwa ya mafanikio ya nchi katika sekta
zote za maendeleo ni kuendelea kuimarika kwa hali ya amani na utulivu nchini.
Alisema
katika kipindi chote cha miaka mitano, Idara maalum za SMZ, Serikali ya Zanzibar
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimetekeleza vyema jukumu lao la
kusimamia ulinzi, amani na utulivu kwa kuhakikisha maisha ya watu na mali zao
yamekuwa salama.
MUUNGANO.
Akizungumzia
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Dk. Shein, alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Awamu ya Saba inatambua na inazingatia haja ya kuimarisha Muungano wa
Tanzania kama nguzo ya pili muhimu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya
mwaka 1964 kwa malengo yale yale ya waasisi wa Muungano huo.
Alisema ni
dhahiri kuwa nguzo hizo za Mapinduzi na Muungano ndizo zimewezesha kupiga hatua
kubwa za maendeleo kisiasa, kiuchumi na kijamii na kuleta heshima ya
Wazanzibari na Watanzania mbele ya mataifa mbali mbali katika kipindi cha miaka
51.
Alisema katika
kipindi hiki cha miaka mitano, Muungano huo umezidi kuimarika kutokana na hatua
zinazochukuliwa na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
UCHIMBAJI WA
MAFUTA NA GESI.
Alisema
amefurahi kuona kuwa Baraza hilo la Nane
limejadili kwa kina suala la uchimbaji wa mafuta na gesi na limeweza kutoa
michango na kuishauri serikali kwa namna mbali mbali kuhusiana na suala hilo.
Alisema hivi sasa wamefikia pazuri hasa ikizingatia kuwa Katiba inayopendekezwa
imezingatia matakwa ya Zanzibar juu ya suala hilo.
Chanzo:-
NIPASHE.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment