Kufunga ni
jambo kongwe na linafanywa na wafuasi wa dini mbalimbali na makundi mengine ya
watu. Sababu za kufunga ni nyingi, miongoni ni kufuata mafundisho ya dini au
ushauri wa daktari. Wiki hii Waislamu wameanza kufunga Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani.
Wafungaji
hao wanajizuia kula kwa takriban saa 14, kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa
12.30 jioni. Wafungaji katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wana milo mikubwa
miwili, mlo wa futari na ule wa daku. Mlo wa futari ni ule ambao mfungaji
anautumia ili kufungua kinywa mara tu jua linapozama.
Kwa kuwa mtu
amekaa muda mrefu bila ya kula chakula, ni vema futari yake iwe mlo laini ambao
ni rahisi kusagwa tumboni. Pia, vyakula hivyo viwe vitamu kutokana na sukari
iliyomo katika vyakula vyenyewe.
Tende,
maziwa, maji, chai, uji, juisi ya asili, ndizi zilizoiva na kupikwa, magimbi,
maboga, viazi vitamu, maharage na mihogo ni baadhi ya vyakula laini vinavyofaa
kutumika kama futari.
Tende ina
asilimia 60 mpaka 70 ya sukari aina ya glukozi na fructose. Mtu akila tende
aina hii ya sukari inanyonywa na utumbo na kuunguzwa na seli na hatimae inatoa
nguvu kwa haraka. Kwa mfungaji saumu, nguvu hii humpa furaha na akili yake
inatuama kwa haraka.
Tende ina
protini asilimia 2.5 na madini asilimia 2.1. Pia, ina mafuta kiasi kidogo
(asilimia 0.4) ili kukidhi haja ya mwili na haina aina mbaya ya mafuta
inayoitwa lehemu.
Zaidi ya
hayo, tende ina nyuzi lishe asilimia 3.9%. Nyuzi lishe zinanyonya sumu kutoka
tumboni na zinasaidia mtu kupata choo kikubwa mara kwa mara hivyo ananusurika
na tatizo la kukosa choo na ugonjwa wa kansa ya utumbo. Tende pia ina vitamini
za aina mbalimbali.
Mlo wa
futari lazima uwe mlo kamili, wenye mafungu yote ya vyakula kama vile wanga,
mafuta, protini, madini, vitamini, maji ya kunywa na nyuzi lishe (dietery
fibles).
Kwa hiyo,
futari ya mihogo au viazi lazima iwe na maharage, nyama, samaki au dagaa. Vilevile,
lazima futari hiyo iwe na matunda na mboga za majani za kutosha.
Vyakula vya
futari na daku visiwekwe sukari, chumvi wala mafuta mengi. Mafuta yanayotokana
na mimea na kwa kiasi kidogo. Mawese, alizeti, ufuta, mahindi ni miongoni mwa
mafuta bora kabisa kwa afya ya mlaji.
Vyakula
vyenye chumvi nyingi au vinywaji aina ya koka, chai na kahawa na vile vyenye
sukari nyingi viepukwe au vitumiwe mara chache usiku wa Ramadhani.
Vyakula na
vinywaji hivyo humfanya mfungaji kupoteza maji mengi panapo kucha kwa njia ya
mkojo. Hali hiyo ni hatari kiafya.
Daku ni
chakula kinacholiwa usiku wa manane kwa ajili ya kujiandaa kufunga siku
inayofuata. Vyakula vizuri kwa daku ni vile vinavyokaa tumboni kwa muda mrefu
(kiasi cha saa 6 - 8). Mfano wa vyakula hivyo ni ngano, shahiri, mtama,
mahindi, mchele, maharage na kunde.
Vilevile,
nyama, samaki, maji ya kunywa, matunda na mboga za majani lazima ziwe sehemu ya
mlo wa daku.
Mama
mjamzito, mama anayenyonyesha, wagonjwa wa kisukari, wenye Virusi Vya Ukimwi
(VVU) na wazee wanatakiwa kupata ushauri kwa wataalamu kabla ya kuanza kufunga.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment