Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ugongo kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Mkuu wa
Tanzania, Mufti Issa Shaaban bin Simba, aliezikwa leo Juni 16, 2015 kwenye
Makaburi ya Waislam, Nguzo Nane Mkoani Shinyanga.
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete ameongoza maelfu ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga katika mazishi
ya sheikh mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaban Simba yaliyofanyika leo June 16,
2015 katika makaburi ya waislamu ya nguzo nane mjini Shinyanga.
Awali kabla
ya maziko ya sheikh mkuu wa Tanzania, sheikh Issa Shaban Simba dua ya kumuombea
ilifanyika katika msikiti wa ijumaa wa majengo mjini Shinyanga ambapo kabla ya
kuwa Mufti,Marehemu Issa Bin Shaban Simba alikua sheikh wa msikiti huo.
Wakitoa
salamu za rambirambi kwa niaba ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.
Jakaya Mrisho Kikwete, baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria mazishi
hayo wamesema hakika taifa limepoteza kiongozi imara na shupavu ambaye alikua
kiuno kikuu kati ya madhehebu mbalimbali ya dini na serikali kwa ujumla.
Nao baadhi
ya waumini wa dini ya kiislamu mjini Shinyanga wamesema kifo cha Mufti Issa
Simba nipengo kubwa lisiloweza kuzibika kwa haraka kwani alikua kiongozi
mnyenyekevu na pia alikua mwalimu wa kufundisha na kuonya bila kubagua dini
yoyote.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment