MAUAJI YA WATU TISA KANISANI NCHINI MAREKANI:-Mshukiwa akamatwa..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 19, 2015

MAUAJI YA WATU TISA KANISANI NCHINI MAREKANI:-Mshukiwa akamatwa..’’

Dylann Storm Roof baada ya kukamatwa na Polisi ambapo mauaji ya watu tisa ndani ya Kanisa la Waafrika Wamarekani katika eneo la Charleston katika jimbo la Carolina Kusini yanaibua maswali kuhusu sehemu mbaya ya historia ya Marekani.

Roof akiwa chini ya ulinzi.
Dylann Storm Roof akiwa ametiwa pingu.
Roof akiwa na gari aina ya Hyundai alilokimbia nalo baada ya kutekeleza shambulio hilo.
....Akipelekwa katika Uwanja wa Ndege tayari kusfirishwa kwenda gerezani.
Waumini wa kanisa la Methodist wakifanya maombi, siku ya shambulio.
....Akipandishwa kwenye ndege…..Katika hotuba yake iliyoonyeshwa katika televisheni muda mfupi baada ya polisi kumkamata mtuhumiwa ambaye ni kijana wa kizungu-- Bwana Obama amesema chuki miongoni mwa jamii kwa misingi ya rangi na imani ni kitisho kwa demokrasia ya Marekani na misingi yake.

Amesema mauaji ya watu wengi hayatokei kwa kiasi hiki katika nchi nyingine zilizoendelea, na ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya pamoja katika fikra za Wamarekani kuhusu ghasia zinazosababishwa na matumizi ya silaha.
Kijana wa miaka tisa, Liam Ellern akisaidia kuotoa mauwa kwenye mlango wa kanisa baada la Methodist.
Wahanga wakiwa katika hali ya sintofahamu mara baada ya shambulio hilo kutokea.
Waumini wakiwa katika majonzi.

Carolina Kaskazini, Marekani.

Jeshi la ulinzi la Marekani limemkamata mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa Methodist la kihistoria mjini Carolina Kusini, Dylann Storm Roof, na kumpeleka gerezani kusubiri kufunguliwa mashtaka yanayomkabiri.

Vyombo vya usalama vya Marekani vinasema, Bw. Roof mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa huko Selby Carolina Kaskazini umbali wa maili 250 kutoka eneo ambapo shambulizi hilo lilitekelezwa (Kanisa la Methodist) saa 13 baada ya shambulizi kabla ya kupandishwa ndege na kupelekwa mahabusu.

Maofisa wa Polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami kwa bunduki aliketi katika mkutano wa mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja kabla ya kufyatua risasi na kuwaua wanawake sita na wanaume watatu akiwemo mchungaji wa kanisa hilo usiku Jumatano.

Maofisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki na ubaguzi wa rangi.

Aidha Mwanasheria Mkuu Bi. Lorreta Lynch, amesema Idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa.

Roof alitekeleza shambulio hilo ndani ya kanisa la Emmanuel African Methodist Church maarufu kama AME, kanisa linaloaminika kuwa la zamani zaidi linalotumiwa na watu wa asili ya Afrika nchini Marekani na kuwaua watu tisa wakiwemo wanawake sita na wanaume watatu miongoni mwao akiwa ni mchungaji wa kanisa hilo, Clementa Pinckney.

CHANZO NA DAILY MAIL

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad