MAFANIKIO:- JK awatunuku nishani Kandoro, Balozi wa Tanzania UN. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 24, 2015

MAFANIKIO:- JK awatunuku nishani Kandoro, Balozi wa Tanzania UN.

Rais Jakaya Kikwete amewatunuku nishani mbalimbali viongozi na watu 28 wakiwamo waliolitumikia Taifa kwa muda mrefu na kwa maadili mema, Waliotunukiwa Nishani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania daraja la Kwanza ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (Pichani), Parseko Kone, Liberata Mulamula na Tuvako Manongi.

Hafla ya kutunuki nishani hizo ilifanyika jana June 23, 2015 katika ukumbi wa mikutano Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi na wananchi.
Nishani zilizotolewa ni nishani ya daraja la kwanza ambayo ilitolewa kwa wananchi waaminifu ambao walijitolea moja kwa moja na kulipatia Taifa sifa kubwa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na kijamii.

Nishani nyingine ni ya utumishi mrefu na maadili mema daraja la kwanza ambayo ilitolewa kwa watendaji wakuu walio hai kwenye utumishi wa umma kuanzia ngazi ya wakurugenzi ambao wametumikia si chini ya miaka 20 mfululizo wakiwa maafisa wandamizi na walioonyesha maadili mema.

Nishani ya utumishi wa muda mrefu na maadili mema daraja la pili ilitolewa kwa watumishi wa umma waliofanya kazi bora na maadili mema yaliyostahili kuigwa na wengine kwa muda usiopungua miaka 20.

Nishani ya ushupavu ilitolewa kwa majeshi ya ulinzi na usalama na watu wengine kwa vitendo vya ushupavu.

Nishani ya utumishi mrefu na maadili mema daraja la kwanza ilitolewa kwa Kipenka Mussa, Florens Turuka, Mbaraka Abdulwakil, Sophia Kaduma, Hab Mkwizu, Rajab Gamaha, Peniel Lyimo, Idris Kikula na Eliakim Mrema.

Nishani ya utumishi mrefu na maadili mema daraja la pili ilitolewa kwa Emmanuel Funto, Agatha Swai, Scolastica Mwibale, Mariam Sauri, Wilberforce Kikwasi, Maria Buchard, Merina Ngoleka, Rosalia Massay na Kapalala Saganga.

Wengine ni Moses Swai, Getrude Kulindwa, Didas Issuja, Asumpta Mbawala na Katembo Msikilwa.

Nishani ya ushupavu ilitolewa kwa CPL Liberatus Ndyetabula.

 Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad