MAADILI YETU:-Mavazi yaliyotamba Kili Music Awards 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 21, 2015

MAADILI YETU:-Mavazi yaliyotamba Kili Music Awards 2015.

Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu ambaye usiku huo alivaa gauni refu la rangi ya kijani.  

Usiku wa tarehe 13, Juni 2015 ulikuwa ni usiku wa Tuzo za Kilimanjaro Muziki (KTMA) na washiriki walionyesha mavazi mbalimbali.

Vazi lililokuwa gumzo katika siku hiyo ni lile alilokuwa amevaa mlimbwende mashuhuri ambaye aliwahi kushinda mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu ambaye usiku huo alivaa gauni refu la rangi ya kijani lilonakshiwa na kitambaa cha resi.

Gauni hilo lilobuniwa na mbunifu kutokana hapa nchini mwanamama Eve Rugemalila maarufu kama Eva Collection.
Wengine walipendeza katika usiku huo ni Joketi Mwegelo maarufu kama Kidoti ambaye alivaa gauni refu lenye kungaa ambalo lilifunika mpaka kicha chake.
Sambamba na hao mrembo Kajala nae alivalia gauni yeusi ambalo lilochanwa kiasi kikubwa na kufanya sehemu ya mwili wake kuonekana,

Mrembo mwengine aliyeonekana kivutio katika usiku huo ni aliyekuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo mwanadada DJ Fetty ambaye alivaa magauni mawili tofauti yaliyoonekana kumpendeza tofauti na alivyozoeleka na wapenzi wake mara nyingi huonekana akivaa mavazi ya suruali na fulana.

Msanii Vanessa Mdee naye alikuwa kivutio katika usiku huo ambapo alivalia gauni refu la rangi ya pinki liloonyesha sehemu kubwa ya mapaja yake huku sehemu ya matiti nayo ikibaki wazi.

Imeandaliwa na Tausi Mbowe- Barua pepe tmbowe@tz.nationmedia.co.tz


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad