Kocha Mkuu
wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars), Rogasian Kaijage
ametangaza kikosi cha wachezaji 30 kitakachoingia kambini siku ya Jumapili
kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya Zambia mwezi Machi mwaka
huu 2015.
Kaijage
ametangaza program yake ya mazoezi
itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari
kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku
akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye
mchezo wa awali.
Twiga Stars
ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF
zilizopo Karume, imeingia moja kwa moja
katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika
msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Wachezaji
walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan,
Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili,
Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad, Anastazia Anthony,
Shelder Boniface.
Wengine ni
Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa,
Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah, Ziada
Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa Haji Vuai (JKU –
Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.
|
No comments:
Post a Comment