LIGI KUU VODACOM 2014/2015:- Matokeo mechi za leo Jumapili Februari 22,2015 kwa Yanga sasa kuwa Pointi 4 mbele ya Azam FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 22, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:- Matokeo mechi za leo Jumapili Februari 22,2015 kwa Yanga sasa kuwa Pointi 4 mbele ya Azam FC.

Taswira ya Mashabiki wa Stand United na Simba SC waliamua kurushiana  makonde uwanjani baada ya shabiki wa Simba (Aliyevaa nguo nyekundu kulia) kukatisha katika jukwaa la mashabiki wa Stand United jioni ya leo Februari 22,2015 katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2014/2015 mzunguko wa pili Stand United ya Shinyanga imecharaza Simba SC bao 1 – 0 .
Katika Mechi nyingine ,Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga SC, Nao leo hii Februari 22,2015,majira ya jioni huko Sokoine, Jijini Mbeya wamepaa kileleni wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili na Mabingwa Watetezi, Azam FC baada ya kuichapa Mbeya City Bao 3-1.

Magoli ya Yanga SC yamefungwa na Simon Msuva, Mrisho Ngassa na Amiss Tambwe, wakati lile la Mbeya City likifungwa na Peter Mapunda.

Mechi ya mwisho hii Leo ilichezwa Usiku wa saa mbili huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kati ya Azam FC na Tanzania Prisons na kutoshana nguvu ya bila kufungana 0 - 0.

MATOKEO VPL 2014/2015.

Jumamosi Februari 21,2015.

Kagera Sugar 1 – 0 Polisi Moro

Ndanda 1 – 0 Coastal Union

Mgambo JKT 1 – 0 Mtibwa Sugar

MSIMAMO LIGI KUU VODACOM 2014/2015.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
 A
 
GD
PTS
1
Yanga
15
9
4
2
21
8
 
13
31
2
Azam FC
14
7
5
2
22
12
 
10
27
3
Kagera Sugar
16
6
6
4
13
11
 
2
24
4
Simba
15
4
8
3
15
12
 
3
20
5
Ruvu Shooting
15
5
5
5
10
11
 
-1
20
6
Mtibwa Sugar
15
4
7
4
15
15
 
0
19
7
Coastal Union
16
4
7
5
10
10
 
0
19
8
JKT Ruvu
15
5
4
6
14
15
 
-1
19
9
Polisi Moro
16
4
7
5
12
14
 
-2
19
10
Ndanda FC
16
5
4
7
14
18
 
-4
19
11
Stand United
16
4
6
6
14
18
 
-4
18
12
Mbeya City
15
4
5
6
10
14
 
-4
17
13
Mgambo JKT
14
5
2
7
8
15
 
-7
17
14
Tanzania Prisons
14
1
8
5
10
15
 
-5
11

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

LIGI KUU VODACOM RATIBA.

Jumamosi Februari 28,2015.

Mbeya City v Ruvu Shooting

Mgambo Shooting v Coastal Union

Simba SC v Tanzania Prisons

Stand United v Kagera Sugar

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad