LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Picha Liverpool ikishinda 2 - 0 na sasa alama moja na timu za Arsenal ,Manchester United na Southampton. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 23, 2015

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Picha Liverpool ikishinda 2 - 0 na sasa alama moja na timu za Arsenal ,Manchester United na Southampton.

Hapo jana Februari 22,2015, Liverpool imeibuka na Point 3 muhimu na kufanya kuwa na pengo la alama moja na timu za Arsenal ,Manchester United na Southampton baada ya mchezaji  Raheem Sterling kuifungia timu yake bao la pili katika ushindi wa 2- 0 dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa St Mary's.

Bao lingine la Liverpool katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England lilifungwa na Phillipe Coutinho.


Nao West Ham hapo jana Februari 22,2015, wakicheza Ugenini huko White Hart Lane, waliongoza kwa Bao 2-0 lakini Wenyeji Tottenham Hotspur walizinduka na kurudisha Bao zote huku Bao lao la Pili likifungwa na Harry Kane katika Dakika za Majeruhi, baada ya Penati aliyopiga mwenyewe kuokolewa na Kipa Adrian na kumrudia yeye na kufunga kwenye Mechi ya Kwanza ya Ligi Kuu Uingereza.

West Ham walitangulia kufunga Bao 2 kwa Bao za Cheikhou Kouyaté, Dakika ya 22, na lile la Dakika ya 62 la Diafra Sakho lakini Spurs wakapata Bao lao la Kwanza Dakika ya 81 Mfungaji akiwa Beki Danny Rose.

RATIBA EPL 2014/2015.

Jumamosi Februari 28,2015.

1545 West Ham v Crystal Palace  
     
1800 Burnley v Swansea
  
1800 Man United v Sunderland  

1800 Newcastle v Aston Villa  
   
1800 Stoke v Hull  

1800 West Brom v Southampton 
         
Jumapili Machi 01,2015.

1500 Liverpool v Man City    
     
1705 Arsenal v Everton    
UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad