KATIBA PENDEKEZWA:-Taswira Mkuu wa Mkoa wa Kagera akizindua na Kusisitiza kila Mtu aipigie kura kwa Mapenzi yake. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 23, 2015

KATIBA PENDEKEZWA:-Taswira Mkuu wa Mkoa wa Kagera akizindua na Kusisitiza kila Mtu aipigie kura kwa Mapenzi yake.

Katika uzinduzi huo, ulioudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kisiasa, Kidini, Ulinzi na Usalama mkoani Kagera, Mkuu wa mkoa wa Kagera,Bw.John Mongela amesema kuwa hakuna kinachoweza kuwa kimekamilika kwa asilimia mia moja, hivyo kutokana na mtazamo na jinsi mwananchi atavyoisoma na kuielewa Katiba Pendekezwa,ndivyo aelekeze kura yake.

Aidha Waziri  wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, amesema kila Kata nchini, itapata nakala 300 za Katiba inayopendekezwa na kwamba tayari serikali imeshaanza kuisambaza,ambapo kuna zaidi ya kata 3,800 nchini kote na lengo la Serikali kuhakikisha inasambaza nakala hizo kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa, wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri za miji, manispaa na majiji.





Tayari Serikali ya Tanzania imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika kura ya maoni iliyopangwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu,2015,kati ya nakala hizo, nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania Bara na nakala 200,000 zinasambazwa Zanzibar.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, mkoa wa Kigoma umepata nakala 41,440 na  Kagera nakala 54,340 na kwamba Idadi ya nakala ya Katiba inayopendekezwa kwa kila mkoa inategemea na wingi wa kata katika mkoa.BOFYA HAPA KUTAZAMA PICHA ZAIDI WAKATI WA UZINDUZI HUO.


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad