PAPA FRANCIS :-Ataka AMANI DUNIANI..Asema“ machozi ni mengi katika siku ya Krismasi” - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 26, 2014

PAPA FRANCIS :-Ataka AMANI DUNIANI..Asema“ machozi ni mengi katika siku ya Krismasi”

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia, Papa Francis amewaongoza maelfu ya waumini wa Kanisa hilo katika misa ya sikukuu ya Krismas Desemba 25,2014 huku akilaani na kukemea vikali vurugu na uhasama dhidi ya wachache katika makundi ya kidini na kikabila hasa nchini Iraq na Syria. 

Kama kawaida yake ya kila mwaka katika siku ya Krismasi, Papa Francis akitoa baraka zake ” urbi et orbi” ikimaanisha kwa mji wa Roma na dunia, amewataka waumini wa Kanisa Katolika duniani kuhubiri amani, akibaini kwamba machozi ni mengi katika siku hii ya Krismasi.


Kama zinavyoeleza mila na desturi za Kanisa katoliki, Papa alionekana katika loggia ya kati ya Basilica St Petro katika mji wa Roma, kabla ya kutoa baraka zake " urbi et orbi".

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki ametoa hotuba yake ya Krismasi mbele ya umati wa waumini wa Kanisa Katoliki. Hotuba yake imerushwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni mbalimbali duniani.

Ikiwa ni mwaka wa pili akisheherekea Krismasi baada ya kukabidhiwa madaraka ya kuliongoza Kanisa Katoliki, Papa Francis ametoa baraka zake kwa watu wote duniani, akianza kwa wale wanaokabiliwa na machafuko ya kivita, mauaji, utumwa na mengineyo.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amelani vikali mateso ya kikatili yanayotekelezwa dhidi ya wakristo wachache nchini Iraq na Syria. Amekaribisha jitihada za wale wote waliojikita kwa kuzikutanisha Israel na Plestina kwenye meza ya mazungumzo.

Papa Francis amependekeza kusitishwa moja kwa moja kwa mvutano unaoendelea kushuhudiwa nchini Ukraine, huku akizitaka nchi nyingi barani Afrika kama Nigeria au Jamhuri ya Afrika ya Kati kudumisha amani.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki ametoa pia baraka zake kwa wagonjwa hususan wale wanaokabiliwa na virusi vya Ebola.

Papa Francis ameelezea masikitiko kuona watoto wamekua wakilengwa katika machafuko mbalimbali, huku akilaani vikali biashara ya watoto. “ Kwa kweli, kwa siku ya leo Desemba 25, machozi ni mengi”, amesema Papa Francis.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad