Tangu
atangazwe aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu mengi yameongelewa
kuhusiana na tetesi za udanganyifu wa umri na vitu vingine kadhaa vinavyomhusu
mrembo huyo ikiwemo suala la umri wake na kiwango cha elimu yake ambapo yeye
mwenyewe alikanusha taarifa hizo.
Story
ikaendelea Novemba 8, 2014 siku ambayo Kamati ya Miss Tanzania ilikutana
na waandishi wa habari Dar es salaam na kutangaza kwamba Sitti Mtemvu ameandika
barua kwa hiari yake yeye mwenyewe, kwamba amelivua taji hilo hivyo kamati hiyo
ikamtangaza Lilian Kamazima aliyekuwa mshindi wa pili kushikilia taji
hilo.
December
25 kuna taarifa kwamba Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka
miwili kutokana na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea,
ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.
Maamuzi hayo
yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey
Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini
ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na
kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.
“Baada ya
kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni vyema
tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea arejee kwa
nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa…“– Mngereza.
Shindano
hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji
warembo wasiokidhi vigezo.
Chanzo
cha Habari: Gazeti
la Mtanzania, December 25,2014.
|
No comments:
Post a Comment