LIGI KUU VODACOM 2014/2015:- Mtibwa Sugar yaingua Azam FC kileleni ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mgambo leo October 05,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 05, 2014

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:- Mtibwa Sugar yaingua Azam FC kileleni ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mgambo leo October 05,2014.

Kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake. Ambapo Hii Leo October 05,2014, huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga SC wameichapa JKT Ruvu Bao 2-1 na kukwea hadi Nafasi ya 3 ya Ligi Kuu Vodacom
Yanga walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 32 kupitia Kelvin Yondani na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.

 Dakika ya 73, Haruna Niyonzima aliipatia Yanga SC Bao la Pili lakini JKT Ruvu walipata Bao lao moja katika Dakika za mwishoni Mfungaji akiwa Jabir Aziz.




Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Kelvin Yondani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha zote na Francis Dande.

Nao Mtibwa Sugar imeiengua Azam FC kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mgambo ya Tanga Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro jioni ya leo October 05,2014.

Matokeo hayo  yanaifanya timu hiyo itimize pointi 9 baada ya mechi tatu, awali ikizifunga Yanga SC 2-0 na Ndanda FC 3-1. 

Bao lililoipandisha kileleni Mtibwa Sugar leo limefungwa na Ally Shomary dakika ya 10 ya mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwa pointi zake 7 ilizovuna katika ushindi wa mechi mbili 3-1 na Polisi Moro, 2-0 na Ruvu Shooting na sare ya 0-0 na Prisons jana mjini Mbeya.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad