LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Pamoja na Chelsea kuifumua Arsenal 2-0 , Jose Mourinho na Arsene Wenger wakwaruzana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 05, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Pamoja na Chelsea kuifumua Arsenal 2-0 , Jose Mourinho na Arsene Wenger wakwaruzana.


Chelsea imeichapa Arsenal mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Uingereza leo October 05,2014 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London na kuwafanya waendelea kujichimbia kileleni mwa Ligi.
 Mechi hii ilichelewa kuanza kwa Dakika 15 kwa sababu za kiusalama baada ya baadhi ya Mashabiki kurusha Fataki kabla Mechi haijaanza.

Pia Mechi ilijaa vituko kibao ikiwa ni pamoja na makocha Jose Mourinho na Arsene Wenger , kukwaruzana wakati Wenger alipochukizwa baada ya Mchezaji wake Alexis Sanchez kuchezewa Rafu na Gary Cahill ambae alipewa Kadi ya Njano na Refa Martin Atkinson.

Chelsea walilazimika kumbadili Kipa wao Courtois katika Dakika ya 24 na kumwingiza Petr Cech baada ya Kipa huyo kugongana na Alexis Sanchez muda mfupi kabla.



Player Team Total goals after first seven Premier League games
Mick Quinn
Coventry City (1992-93)
10
Diego Costa
Chelsea (2014-15)
9
Sergio Aguero
Manchester City (2011-12)
8
David White
Manchester City (1992-93)
7
Jurgen Klinsmann
Tottenham Hotspur (1996-97)
7
Francesco Baiano
Derby County (1997-98)
7
Papiss Cisse
Newcastle (2011-12)
7

Chelsea walifunga Bao lao la kwanza katika Dakika ya 27 kwa Penati ya Eden Hazard iliyotokana na Laurent Koscienly kumchezea Rafu Hazard na kupewa Kadi ya Njano.

Dakika ya 77, bonge la Pasi ndefu ya Fabregas mbele ilishushwa kifuani na Diego Costa na kukabiliana na Kipa Szczesny na kumvisha kanzu kuandika Bao la Pili kwa Chelsea.




Sasa Chelsea imekwea kileleni mwa Premier League na pointi 19 huku Costa akizidi kupaa kwa wafungaji bora akiwa na mabao tisa.

Jumamosi Oktoba 18,2014.

1445 Man City V Tottenham

1700 Arsenal V Hull

1700 Burnley V West Ham

1700 Crystal Palace V Chelsea

1700 Everton V Aston Villa

1700 Newcastle V Leicester

1700 Southampton V Sunderland


Jumapili Oktoba 19,2014

1530 QPR V Liverpool

1800 Stoke V Swansea

Jumatatu Oktoba 20,2014

2200 West Brom v Man United

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
MSIMAMO EPL 2014/2015.


NA TIMU P GD PTS
1 Chelsea 7 14 19
2 Man City 7 7 14
3 Southampton 7 6 13
4 Man United 7 3 11
5 Swansea 7 2 11
6 Tottenham 7 2 11
7 Arsenal 7 2 10
8 Liverpool 7 0 10
9 Aston Villa 7 -5 10
10 Hull 7 0 9
11 Leicester 7 -1 9
12 Sunderland 7 1 8
13 West Brom 7 -1 8
14 Crystal Palace 7 -2 8
15 Stoke 7 -2 8
16 West Ham 6 0 7
17 Everton 7 -3 6
18 Newcastle 7 -7 4
19 Burnley 7 -7 4
20 QPR 6 -9 4

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad