Maandamano
ya walimu kuingia katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya
Walimu Duniani, jana October 05,2014 ambapo yalipata mtafaruku baada ya Polisi
kuyaingilia na kuchana bango mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge la
Katiba.
Bango hilo
la kitambaa cheupe lilikuwa na maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000
waliyokuwa wanapata wajumbe wa Bunge la Katiba, yakilinganishwa na kazi kubwa
wanayofanya walimu.
Ujumbe
wenyewe ulisomeka hivi: “Haki iko wapi usawa uko wapi, posho ya mjumbe wa Bunge
la Katiba kwa siku shilingi laki tatu, mshahara wa mwalimu shilingi 370 kwa
mwezi. No big results without big salary (Hakuna matokeo makubwa bila mshahara
mkubwa)”.
Ujumbe huo
ulikuwa ukifanya rejea ya viwango vya malipo ya Sh300,000 kwa siku ambazo walikuwa
wakilipwa wajumbe wa Bunge Maalumu zikiwa ni Sh230,000 kama posho ya kujikimu
na Sh70,000 ambazo ni posho ya vikao.
Hata hivyo
bango hilo lilichanwa hatua chache kabla ya walimu hao hawajaingia uwanjani
humo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu,Bw. Mizengo Pinda.
|
No comments:
Post a Comment