LIGI KUU UINGEREZA 201/2015:-Matokeo ya Manchester United vs Everton 2-1 sasa yapanda hadi Nafasi ya 4 katika Msimamo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 05, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 201/2015:-Matokeo ya Manchester United vs Everton 2-1 sasa yapanda hadi Nafasi ya 4 katika Msimamo.

Manchester United wakicheza Uwanjani kwao Old Trafford wameifunga Everton Ba0 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza leo October 05,2014 huku Kipa wao David De Gea akiwa Shujaa kwa kuokoa Penati na Bao kadhaa lakini aliewapa ushindi ni Straika Radamel Falcao aliefunga Bao la Pili na la ushindi na hilo ni Bao lake la kwanza kwa Man united.

 Man United walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 27, Angel Di Maria alipofunga Bao safi kufuatia Krosi ya Rafael kuokolewa na Jagielka na Mpira kumfikia Juan Mata aliemsogezea Di Maria na kufunga.

Dakika ya 47, baada ya Dakika 2 kuongezwa kwenye Kipindi cha Kwanza, Refa Kevin Friend aliwapa Everton Penati kwa madai Luke Shaw amemwangusha Tony Hibbert na Penati hiyo kupigwa na Leighton Baines ambae hadi sasa amefunga Penati 14 kati ya 14 alizopiga kwenye Ligi Kuu England lakini hii Leo alikosa baada Kipa David De Gea kuokoa vizuri.

Everton walisawazisha Dakika ya 55 kwa Bao la Steven Naismith alipounganisha kwa Kichwa kufuatia Krosi ya Leighton Baines.

Dakika ya 62, Krosi ya Angel Di Maria iliunganishwa vizuri Radamel Falcao na kufunga Bao lake la kwanza kwa Man United na kuifanya Timu yakr iongoze 2-1.

Mwishoni mwa Mechi hii, Kipa wa Man United aligeuka shujaa kwa mara nyingine kwa kuokoa Bao 2 za wazi.
MSIMAMO EPL 2014/2015.

NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
6
12
16
2
Man City
7
7
14
3
Southampton
6
7
13
4
Man United
7
3
11
5
Swansea
7
2
11
6
Arsenal
6
4
10
7
Liverpool
7
0
10
8
Aston Villa
7
-5
10
9
Hull
7
0
9
10
Leicester
7
-1
9
11
Sunderland
7
1
8
12
Tottenham
6
1
8
13
West Brom
7
-1
8
14
Crystal Palace
7
-2
8
15
Stoke
7
-2
8
16
West Ham
6
0
7
17
Everton
7
-3
6
18
Newcastle
7
-7
4
19
Burnley
7
-7
4
20
QPR
6
-9
4
 
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad