Zitto Kabwe aweka pingamizi Mahakamani kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kumjadili kesho(Januari 03,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 02, 2014

Zitto Kabwe aweka pingamizi Mahakamani kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kumjadili kesho(Januari 03,2014.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo(Januari 02,2014), ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kutojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia kufanyika kesho, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando.



Kwa maneno yake Zitto Kabwe: "Nimeomba mahakama kuzuia kamati kuu ya chama changu kunijadili mpaka rufaa yangu isikilizwe na Baraza Kuu la chama. Sijaomba kuzuia kamati kuu kuendelea na kikao chake.

Nimeomba kamati isinijadili maana nina rufaa kwenda Baraza Kuu kwa jambo hilo hilo ambalo kamati kuu inataka kuliamulia.

Wakili  wa chama Tundu Lissu aliweka mapingamizi akisema mahakama haina mamlaka kujadili masuala ya vyama na wanachama wao.
 Jaji John Utumwa katupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu.

 Mahakama ndio Chombo cha kutoa haki.

Asante Wakili Albert Msando.

Haki itatendeka…"

Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad