Waziri wa
Fedha William Mgimwa ,
enzi za uhai
wake.
|
Waziri wa
Fedha, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Iringa, William Mgimwa amefariki
dunia leo(Januari 01,2014) akiwa hospitali ya Mediclinic Kloff, Afrika Kusini
alipokuwa akitibiwa!
Taarifa za
kifo chake zimethibitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, ambaye amesema
Mgimwa amefariki majira ya saa 5:20 saa za Afrika Kusini ambapo ni sawa na saa
6:20 kwa majira ya Tanzania.
Marehemu
Mgimwa alizaliwa Januari 20, 1950 na amefariki akiwa na umri wa miaka 63.
Alipata
Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) na Stashahada ya Uzamili (Postgraduate
Diploma) katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.
Alisoma
Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Fedha (MBA) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe
mkoani Morogoro.
MUNGU AILAZE
ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
No comments:
Post a Comment