Mtoto Rehema
akiwa huru baada ya kuokolewa na majirani.
|
MAMBO YALIPOANZA
KUTIBUKA.
Wiki
iliyopita, watoto hao waliokolewa na majirani katika kifungo cha miezi sita
ndani huku afya zao zikiwa zimedhoofu kwa kukosa chakula.
Ilidaiwa
kwamba, watoto hao Hassan na Hussein ambao ni mapacha na Rehema, walifungiwa katika banda la shangazi yao
aitwaye Asia Bora ambalo ujenzi wake haujakamilika. Wamekuwa wakiishi humo kwa
kula mabaki ya vyakula jalalani.
USHUHUDA WA
MAJIRANI.
Wakizungumza
na gazeti hili hivi karibuni, majirani wa nyumba hiyo walimweleza mwandishi
wetu kuwa watoto hao wamekuwa
wakionekana nje ya nyumba hiyo mara
chache sana wakiwa wanagombania mabaki ya vyakula kwenye jalala.
Banda walimokuwa wakiishi watoto hao. |
“Tumekuwa
tukiwaona nje mara chache kwenye jalala. Unajua, Asia (shangazi yao) aliwachukua
kwa kaka yake, Kijiji cha Namakongoro Kata ya Lihimalyao huko Kilwa mkoani
Lindi.
“Tukasikia
lengo lake aje kuishi nao kwa vile yeye Mungu hamkujalia kupata watoto.
Lakini
maisha hapo kwake yakawa siyo mazuri kwa kipato kwa mama huyo.
Mmoja wa
majirani hao aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Ramadhan yeye alikwenda mbele
zaidi kwa kusema.
“Hapo awali
tulikuwa tukiwaona wakitoka nje na kucheza na watoto wetu huku wakiwa na afya
nzuri. Asia akatueleza kuwa ni watoto wa nduguye, amewachukua huko kijijini.
“Baada ya
muda fulani tukawa hatuwaoni, tulidhani amawarudisha kwao, lakini kadiri siku
zilivyokuwa zinakwenda mbele tukawa tunawaona mara chache wakiwa jalalani
wanapigania mabaki ya chakula.
“Kuna siku
mimi niliwakamata wakiwa wamebeba mfuko wa rambo wenye kinyesi, walikuwa
wanakuja kutupa katika maeneo yetu, nikawarudisha nao kwa shangazi yao. Kumbe
nyumba wanayoishi haina choo ndiyo maana wamekuwa wakijisaidia kwenye rambo.
“Siku moja
walipotoka nje kutafuta chakula jalalani, mimi na majirani wenzangu tuliwauliza
wanaishije? Wakatuambia hawapewi chakula na shangazi yao akitoka asubuhi harudi
mapema, akirudi inakuwa ni usiku sana wao wakiwa wameshalala.
Ndani ya
banda walimokuwa wakiishi watoto hao.
|
“Inasikitisha
sana kuwaona watoto hawa wanaachwa peke yao kutwa nzima bila mtu wa kukaa nao
na wamekuwa wakifungiwa ndani kwa muda mrefu sasa, ila huwa wanakiuka masharti
na kutoka kwa ajili ya kutafuta mabaki ya chakula.
Jirani huyo
akaendelea kuanika mateso ya watoto hao: “Kwa kuwaonea huruma tumekuwa tukilazimika
kuwapa chakula, lakini Asia anaporudi na kugundua hilo anawapiga, kwa hiyo
wakawa waoga kuja kuchukua chakula. Mimi niliumia hadi machozi.”
Jirani:
“Baadaye wakawa hawaonekani, lakini cha ajabu mara nyingi tukiamka asubuhi
tunakuta mifuko ya rambo yenye vinyesi imetapakaa, tukimweleza Asia inakuwa
ugomvi.
“Siku moja
baada ya shangazi yao kuondoka, nilikwenda kuwachungulia ndani, nikawaona
wamekonda sana, wamepauka na wamevaa nguo zilizochakaa.
“Nilitokwa
machozi, nililazimika kuwaita wenzangu nao walipofika hakuna aliyejizuia kulia.
Tukasema hawa watoto watakufa, ndiyo tukaamua kuwaokoa kwa kupeleka taarifa kwa
mzee Dadi Salum ambaye ni polisi jamii wa hapa.
POLISI JAMII
NAYE ALIA.
“Mzee Dadi
naye alipofika na kuwaona kwa macho alilia, watu wakaanza kukusanyika,
tukawatoa nje watoto, kila mmoja aliwaonea huruma. Tuliwachukua hadi Ofisi ya
Serikali ya Mtaa wa Nzasa A.
SHANGAZI MTU
ANUSURUKA KIPIGO.
“Hatujui ni
nani aliyempigia simu Asia, kwani muda mfupi tu tukasikia yupo nyumbani kwake.
Uongozi wa mtaa ulimfuata, walipofika, wanawake wenzake hasa wale anaochukua
nao mkopo wa fedha benki walitaka kumpiga wakimuuliza pesa anapeleka wapi.
“Hata hivyo
aliokolewa na polisi jamii ambao walimchukua na kumweka katika Bajaj na
kumpeleka Kituo cha Polisi Mbagala kwenye Dawati la Jinsia na Watoto, watoto
nao pia walipelekwa huko.”
Naye
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nzasa A, Mrisho Salum alikiri kuwapokea
watoto hao wakiwa katika hali mbaya kiafya, wakapelekwa polisi. Akawataka
wananchi kutokaa kimya mara wanapoona vitendo kama hivyo.
Mwandishi
alifika hadi kituo cha polisi na kuambiwa na askari mmoja kuwa mapacha
walichukuliwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Othman Mbwana aliyedai ni babu yao.
Mbwana
alidai kwamba ameamua kuwachukua watoto hao wakaishi nyumbani kwake wakati
akifanya mawasiliano na wazazi wao.
“Kwanza
nitawapeleka hospitali wakatazamwe afya zao, ila nimesikitishwa sana na hali
hii, sijajua ni kwa nini watoto hawa wamefikia hatua hii,” alisema Mbwana.
Rehema yeye
alichukuliwa na mjomba wake aitwaye Sood Ismail ambaye alidai anakwenda kukaa
naye hadi hapo atakapofanya mawasiliano na wazazi wa huyo mtoto, akisema
kitendo cha Asia kimeidhalilisha familia.
RPC TEMEKE
ATUPIA NENO.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo amewataka wananchi kufichua vitendo
viovu ndani ya jamii na amewapongeza vijana wake wa ulinzi shirikishi kuokoa
maisha ya hao watoto.
No comments:
Post a Comment