 |
Hili ni Banda linaloendelea kujengwa katika eneo la makazi ya Hayati
Mzee Nelson Mandera kwa ajili ya maandalizi ya shughuli za maziko yanayotarajia
kufanyika mwishoni mwa wiki hii(Desemba 15,2013), ....ambapo zaidi ya viongozi 70 wa mataifa
makubwa, kutoka pande zote za dunia wanatarajia kuhudhuria maziko hayo.
|
 |
Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini ameaga dunia(Desemba 05,2013) . Mandela ameaga akiwa na
umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa
watawala wa enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa
jela kwa miaka 27
Mandela
alikua anpokea matibabu ya homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa
hospitalini kwa miezi mitatu.
|
Mnamo mwaka 2005, Mandela alitangaza kwa taifa kua mwanawe wa kume alifariki
kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini,
Rais wa taifa hilo, Jacob Zuma , alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko
mahali salama.
Rais Zuma
amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela
aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais
aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya
kuondoka gerezani.
Hakuonekana
sana hadharani tangi alipostaafu mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment