Taswira ya sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania bara , mwaka 1961. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 09, 2013

Taswira ya sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania bara , mwaka 1961.

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo (Desemba 09,2013) ameongoza mamilioni ya Watanzania katika kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 tangu Tanganyika kupata uhuru ambayo baadaye iliungana na Zanzibar na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati hayo yakijiri ,hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kusherehekea uhuru wake huku bendera yake ikipepea nusu mlingoti kufuatia msiba mkubwa uliotokea wa kiongozi mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21 kiongozi wa kwanza mweusi nchini Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela aliyefariki dunia mnamo tarehe 5 Desemba 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo Rais Kikwete alitangaza siku 3 za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba 2013 na kuagiza bendera zote kupepea nusu mlingoti.
Picha Juu na Chini ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua Gwaride kwenye Uwanja wa Uhuru leo (Desemba 09,2013), alipojumuika na wananchi kusherehekea miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati alipowasili uwanjani hapo.
Pamoja na mambo mengine,Rais Kikwete akitoa salamu za maadhimisho sambamba na salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandera.
 Rais Kikwete akiwaongoza Viongozi na wananchi kusimama kuimba Wimbo wa Taifa......
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye naye pia leo (Desemba 09,2013) anasherehekea maana halisi ya jina lake kutokana na kuzaliwa mwaka uliopatikana Uhuru wa Tanzania, mwaka 1961........... na ndiyo maana akaitwa Freeman.
Rais Kikwete, akipiga picha ya pamoja na wasaidizi wake na baadhi ya viongozi baada ya chakula cha mchana.
Wake wa viongozi nao wakipata picha ya pamoja ya kumbukumbu...

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad