Mshindi wa
pili wa mbio za kilometa 42 kwa upande wa wanaume, Steven Silvester kutoka
Tanzania akimaliza mbio hizo.
|
Mshindi wa
mbio za km 21 kwa wanawake, Jacqueline Sakilu ambaye ni mwajiriwa wa jeshi
la wananchi wa Tanzania ambae ameshinda na kujinyakulia kiasi cha shilingi
milioni moja.
|
Mbio ndefu
za Uhuru ( Uhuru Marathon ) zilifanyika jana (Desemba 08,2013) kwa kuanzia na
kumalizikia katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam huku
Watanzania na Wakenya wakichuana vilivyo na kugawana nafasi za ushindi.
Katika mbio
za kilomita 42 upande wa wanaume mshindi alikuwa ni Jamini Ikai kutoka Kenya
aliyetumia saa 2:33:35, akifuatiwa na Steven Sylvester wa Tanzania akitumia saa
2:42:05, nafasi ya tatu ilishikwa na Alex Sanka aliyetumia saa 2:44:14 toka
Tanzania pia, akifuatiwa na James Shigela aliyetumia saa 2:47:40 na watano
akiwa Getuni Gumali aliyekimbia saa 2:52:88.
Kwa upande
wa wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Thabita Kibeti wa Kenya
aliyekimbia saa 3:24:50, akifuatiwa na Naumi Jepkosgei wa Kenya pia aliyekimbia
saa 3:45:09 na nafasi ya tatu ilitwaliwa na Banuelia Brighton wa Tanzania
aliyekimbia saa 4:05:36.
Katika
kilomita 21 upande wa wanaume nafasi ya kwanza na pili ilienda Kenya pale
Elijah Tirop alipokimbia kwa saa 1:06:12, akifuatiwa na Wilson Tuitoe
aliyekimbia saa 1:06:38, watatu akiwa Eliah Daudi wa Tanzania aliyetumia saa
1:07: 10, Hilary Kepchumba wa Kenya akishika nafasi ya nne kwa kukimbia saa
1:07: 12 na ya tano ikaenda kwa Wilbert Peter wa Tanzania aliyetumia saa
1:08:56.
Kwa upande
wa wanawake nafasi ya kwanza ilikamatwa na Jacqueline Juma wa Tanzania
aliyekimbia saa 1:15:25:06, Anjela Temu wa Kenya alitwaa nafasi ya pili kwa
kukimbia saa 1:16:01:85, Catherine Range wa Tanzania alikimbia saa 1:17:33:82,
Mary Mangegeia aliyekimbia saa 1:18:26:80 na Agnes Chepete akikimbia saa
1:23:21:85 wote hawa kutoka Tanzania.
Washindi wa mbio ndefu kwa upande wa mbio za kilomita 42 kwa upande wa wanaume na wanawake kila mmoja aliondoka na Sh milioni 2, kwa upande wa mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake kila mmoja alipata Sh milioni 1.
Mshindi wa
pili kilomiita 21 kwa wanaume na wanawake walipata Sh 700,000 huku kilomita 42
wakiondoka na Sh milioni 1 kwa kila mmoja.
Mshindi wa
tatu kilomita 21 kwa wanaume na wanawake kila mmoja alipata Sh 500,000 na
kilomita 42 walipata Sh 600,000 washindi wa nne kwa kilomita 21 na 42 kwa
wanawake na wanaume kila mmoja aliondoka na Sh 300,000 wakati yule aliyeshika
nafasi ya tano kwa kilomita 21 wanawaume alipata Sh 150,000 na kilomita 42
ilikuwa Sh 200,000 huku walemavu kumi wakipata Sh 100,000.
![]() |
Dk. Mohammed Gharib Bilal. |
“Tanzania
imesaidia sana kupigania uhuru wa nchi mbalimbali, hivyo hatuwezi kukubali eti
sisi tugawanyike vipande hiyo haitakubalika na naamini vijana mnaona, mnasikia
na kuwajua wanaoleta chokochoko hizo,” alisema, huku washiriki wakisimama pia
kuomboleza kifo cha Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Awali,
Katibu wa Kamati ya Mbio hizo, Innocent Melleck alitumia pia fursa hiyo kuiomba
Serikali kuwasaidia zaidi, kwani mwakani wanataka kulisambaza katika mikoa
mbalimbali ili kudumisha umoja wa Kitaifa.
“Mheshimiwa
Makamu wa Rais mwakani ni miaka 50 ya Muungano tunatarajia kuanza maandalizi
mapema na tutafanya uzinduzi rasmi Butiama mkoani Mara, ikiwa ni kumuenzi Baba
wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kisha tutafanya matamasha kama hayo katika
kanda sita tofauti kabla ya kumalizia kwenye mbio za Uhuru tarehe 8 Desemba
jijini Dar es Salaam, kwa umemwakilisha Mheshimiwa Rais, tunaomba utuwakilishie
hili kwake ili tupate sapoti ya serikali katika jambo hili la kudumisha Amani
na umoja wa kitaifa tuliorithishwa na waasisi wa taifa hili,” alisema Melleck.
Akijibu
hilo, Makamu wa Rais alimwagiza Katibu Mkuu na Waziri mwenye dhamana ya michezo
kuhakikisha hilo linatekelezeka.
Mbio za
Uhuru zilidhaminiwa na GrandMalt, Konyagi, Kibuku, Mwananchi Communications,
Sayona, CocaCola, KAPARI, Clouds FM, Uhuru FM, TBC 1, TBC Taifa, Integrated
Communications, Night Support, Tindwa Medical, Forever Living na SamSung.
No comments:
Post a Comment