![]() |
Mchezaji Mesuit Ozil akishangilia na wachezaji wenzake wa Arsenal baada
ya kufunga bao.Sasa,
Arsenal wapo juu kwenye Msimamo wa Ligi ya Uingereza wakiwa Pointi 5 mbele ya Liverpool na
Chelsea.
|
![]() |
Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la kuongoza
katika dakika ya 80 ya mchezo.
|
![]() |
Gerard Deulofeu wa Everton (kushoto)
akishangilia bao la kusawazisha dakika ya 81 ya mchezo.
|
![]() |
Beki wa Arsenal Laurent Koscielny (kushoto)
akijaribu kumzuia Steven Pienaar wa Everton wakati wa mchezo huo.
|
Vinara wa
Ligi Kuu Uingereza , Arsenal jana (Desemba 08,2013) wamekatwa makali yao ya kuzidi kuchanja mbuga
kileleni baada kwenda Sare ya Bao 1-1 na Everton Uwanjani Emirates.
Sasa,
Arsenal wapo juu kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa Pointi 5 mbele ya Liverpool na
Chelsea.
Position | Team | Played | Goal Difference | Points |
---|---|---|---|---|
1 | Arsenal | 15 | 19 | 35 |
2 | Liverpool | 15 | 16 | 30 |
3 | Chelsea | 15 | 13 | 30 |
4 | Man City | 15 | 26 | 29 |
5 | Everton | 15 | 9 | 28 |
6 | Tottenham | 15 | -1 | 27 |
7 | Newcastle | 15 | -1 | 26 |
8 | Southampton | 15 | 5 | 23 |
9 | Man Utd | 15 | 3 | 22 |
10 | Aston Villa | 15 | -2 | 19 |
11 | Swansea | 14 | 1 | 18 |
12 | Stoke | 15 | -5 | 17 |
13 | Hull | 14 | -6 | 17 |
14 | Norwich | 15 | -14 | 17 |
15 | West Brom | 15 | -4 | 15 |
16 | Cardiff | 15 | -11 | 14 |
17 | West Ham | 15 | -6 | 13 |
18 | Fulham | 15 | -12 | 13 |
19 | Crystal Palace | 15 | -12 | 13 |
20 | Sunderland | 15 | -18 | 8 |
Hadi
Mapumziko, Timu hizi zilikuwa Droo 0-0 na zikiwa zimebaki takriban Dakika 20,
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, aliamua kuingiza Wachezaji watatu kwa mpigo,
Mathieu Flamini, Tomas Rosicky na Theo Walcott na kuwatoa Santi Cazorla, Aaron
Ramsey na Jack Wilshere.
Mabadiliko
hayo yalileta uhai na katika Dakika ya 80 Tomas Rosicky alipiga krosi
iliyomkuta Theo Walcott ambae nae krosi yake ilishindwa kuunganishwa na Olivier
Giroud na kumdondokea Mesut Ozil aliefunga Bao kwa Arsenal.
Bao hilo
lilidumu Dakika 4 tu kwani Chipukizi alietoka kwa Mkopo Barcelona, Gerard
Deulofeu, mwenye Miaka 19, na alietokea Benchi kuchukua nafasi ya Kevin
Mirallas, alimalizia kazi njema ya Chipukizi mwingine, Ross Barkley,
iliyoshindwa kuunganishwa na Romelu Lukaku baada kuukosa Mpira kwa tikitaka, na
kumkuta Deulofeu aliepiga kifundi na kucheka na kamba.
![]() |
Wenger
encouraged
by Everton draw.
|
Arsenal
wangeweza kuibuka kidedea kwani katika Dakika ya 93, Dakika ya mwisho ya muda
wa Nyongeza wa Dakika 3, Olivier Giroud aliachia mzinga wa Mita 25 uliopiga
besera.
Arsenal,
licha ya kushinda Mechi 4 kati ya 5 katika Kundi F la UEFA, bado wanangoja uhakika kwa
matokeo ya Mechi yao ya mwisho Ugenini huko Italy na Napoli.
Aidha Michuano ya
Vilabu Ulaya UEFA , hatua ya Makundi
inafikia tamati Jumanne na Jumatano, kwa
Mechi za mwisho na tayari Timu 8 zimejihakikishia kuingia Raundi ya Mtoano ya
Timu 16 na bado zipo Nafasi 8.
Timu 8
zilizofuzu ni Mabingwa Watetezi Bayern Munich, Chelsea, Manchester City,
Manchester United, Real Madrid, Paris St-Germain, Barcelona, na Atletico Madrid.
MECHI ZA
MWISHO ZA MAKUNDI
[SAA 4
Dakika 45 Usiku]
Jumanne
10 Desemba 2013.
Manchester
United FC v FC Shakhtar Donetsk
Real
Sociedad de Fútbol v Bayer 04 Leverkusen
Galatasaray
v A.Åž. Juventus
FC København
v Real Madrid CF
SL Benfica v
Paris Saint-Germain
Olympiacos v
FC RSC Anderlecht
FC Bayern
München v Manchester City FC
FC Viktoria
Plzeň v PFC CSKA Moskva
Jumatano
11 Desemba 2013
FC Schalke
04 v FC Basel 1893
Chelsea FC v
FC Steaua BucureÅŸti
Olympique de
Marseille v Borussia Dortmund
SSC Napoli v
Arsenal FC
FK Austria
Wien v Football Club Zenit
Club Atlético
de Madrid v FC Porto
AC Milan v AFC
Ajax
FC Barcelona
v Celtic FC
No comments:
Post a Comment