Gari hilo
baada ya kupinduka.…
|
Baadhi ya
abiria waliokuwa wanasafiri katika basi hilo.
|
Baadhi ya
abiria wakitoa mizigo yao katika basi hilo.
|
Basi hilo
likitolewa eneo la ajali.
|
Baadhi ya
wananchi wakipanda basi lingine la Hood kuendelea na safari kama kawaida.
|
...Baada ya
kutolewa.
|
Eneo la
Melela Mlandizi ilipotokea ajali hiyo.
|
Basi la
kampuni ya Hood Limited aina ya Scania lenye namba za usajili T 159 AXM
lililokuwa likitoka jijini Mbeya kueleka Arusha limepinduka kwenye kona kali
iliyopo eneo la Melela, Mlandizi wilayani Mvomero, Morogoro jana (Desemba 19,2013) majira ya saa
nane mchana na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi 27.
Majeruhi
kadhaa katika ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa
matibabu.
Mashuhuda wa
ajali hiyo walidai kwamba chanzo chake ni dereva wa lori aliyejaribu kulipita
gari lingine kwenye kona hiyo.
"Mimi
nilikuwa natoka Mbeya naenda Moshi kwa ajli ya sikukuu ya Krismas, dereva wetu
amefanya kazi kubwa sana ya kuokoa maisha yetu.
"Tulipofika
hapa kwenye kona, dereva wetu baada ya kuona lori limejaa upande wetu akaamua
kukwepa kugongana nalo uso kwa uso na kuingia huku lilipo. Binafsi nampa
pongezi nyingi dereva wa hili basi letu" alisema Bi. Ruth Mwambogoso
abiria katika basi hilo
(PICHA NA
DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MORORGORO)
No comments:
Post a Comment