Padre Lazaro
Kadende alizaliwa katika kijiji cha Nakatunga wilayani Ngara mwaka 1934 na
kujiunga na elimu ya msingi mwaka 1944 ambapo mwaka 1945 alibatizwa kisha
kujiunga na seminari mwaka 1947 huko Rubya wilayani Muleba na kuendelea 1957
huko Katigondo ya Bukoba.
Mnamo
Januari 1963 alipewa daraja la ushemasi na na mhashamu askofu Joseph Kiwanuka
na tarehe 18 Desemba 1963 alipata daraja la Upadre na kuanza harakati za
kumtumikia Mungu na kuchunga kondoo wake kwa njia za kiroho.
Aidha Padre Lazao Kadende katika utumishi wa daraja
la upadre ametumikia parokia mbalimbali za jimbo la Rulenge Ngara na kuwa
mkurugenzi wa elimu jimboni ,mkurugenzi wa vipindi vya radio na makamu wa baba
Askofu
Nae Baba askofu wa jimbo la Rulenge Ngara ,Mhashamu Severini Niwemugizi ametoa wito
kwa wazazi na walezi kuwapa moyo watoto wao kuwa na miito ya utume kwa kuwapatia mafunzo
ya imani kupitia kwa walimu wa kiroho.
Amesema kuwa
vijana pia watumie elimu na vipaji waliojaliwa na mungu bila kulazimishwa
walitumikie kanisa kwani kazi ya kulitangaza neon la Mungu ni kama kazi
nyingine na mafanikio yake yanajengwa na upendo kuhubiri amani na subira.
No comments:
Post a Comment