![]() |
Majambazi
ambao majina yao hayajafahamika waliokuwa wakipanga kuvamia mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama usiku wa kuamkia leo(Desemba 20,2013).
|
![]() |
Wakiwa
mochwari hospitali ya wilaya ya kahama
|
Watu watatu
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika
kijiji cha Namba Tisa kata ya Bulyanhulu Tarafa ya Msalala wilayani Kahama
mkoani Shinyanga wakati wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu kwenye mgodi wa
dhahabu wa Bulyanhulu.
Watu hao
ambao hawajafahamika majina yao, wana umri wa kati ya miaka 25 na 30.
Kamanda wa
Polisi mkoani Shinyanga, Evarist Mangala (pichani), alisema tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia jana wakati watuhumiwa hao wakiwa katika harakati za
kuvamia mgodi wa dhahabu Bulyanhulu.
Kamanda
Mangala alisema wakati watu hao wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu huo,
walianza kurushiana risasi na polisi.
Hata hivyo,
alisema watu hao walizidiwa nguvu na polisi na kusababisha vifo vyao.
Kamanda
Mangala alifafanua kuwa baada ya kuwaua watuhumiwa hao, polisi walikamata
silaha za kivita yakiwamo mabomu matatu ya kurushwa kwa mkono na bunduki mbili
aina ya Sub Machine Gun (SMG) zenye namba 1972px7482 na ya pili yenye namba
UC-17751998 pamoja na risasi 94 zikiwa kwenye magazine nne.
Alisema watu
hao wanadaiwa walipanga kupora mali katika mgodi huo lakini walikwama baada ya
polisi kupewa taarifa kutoka kwa wanakijiji na kufika eneo hilo.
![]() |
Kamanda wa
Polisi mkoani Shinyanga,
Evarist
Mangala
|
Kamanda
Mangala aliongeza kuwa baada ya kufika eneo la tukio, watuhumiwa hao walianza
kurushiana risasi na polisi lakini walizidiwa nguvu na kuuawa wote.
Aidha,
alisema miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Kahama ikisubiri kutambuliwa na ndugu zao.
Alitoa wito
kwa wananchi mkoani humu kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa
taarifa pale wanapohisi kutokea uhalifu ili kudhibiti matukio hayo mapema.
No comments:
Post a Comment