![]() |
Madaktari wakiwa wameunganisha mkono wa Xiao
kwenye kifundo cha mguu wakisubiri apone majeraha mengine ili waurudishe eneo
lake.
|
![]() |
Madaktari wakiuangalia
mkono wa Xiao Wei kabla ya kumfanyia oparesheni kuurudisha eneo lake.
|
![]() |
Xiao Wei
baada ya kurudishiwa mkono wake. (Picha Zote na Rex).
|
Mkono wa
kulia wa Xiao Wei mkazi wa Changde, Kusini mwa China, uliunganishwa katika
kifundo cha mguu wake kwa mwezi mzima kabla ya madaktari kuurudisha eneo lake.
Mkono wa Xiao ulikatika katika ajali kiwandani alipokuwa kazini.
"Nilishtuka
sana na kushindwa kuondoka eneo hilo mpaka wafanyakazi wenzangu walipoondoa
mashine na kutoa mkono wangu kisha kunipeleka hospitali" Alisema Xiao,
akielezea ajali hiyo iliyotokea mwezi uliopita.
Baada ya
kupelekwa katika hospitali mahiri nchini China, saa saba baada ya ajali hiyo,
madaktari walisema wataurudisha mkono huo ila siyo moja kwa moja.
Ili kuzuia
mkono wa Xiao usiharibike, madaktari waliamua kuuunganisha katika kifundo cha
mguu ambapo ulikaa kwa mwezi mzima baada ya kupona majeraha mengine ndipo
walipourudisha katika eneo lake. Madaktari wanadai Xiao atapona vizuri na mkono
wake utafanya kazi kama zamani.
Source:-
Metro.
No comments:
Post a Comment