![]() |
'I am not a
quitter' - Villas-Boas.
|
Klabu ya Tottenham
Jana(Desemba 16,2013) imemfukuza kazi
Meneja wao Andre Villas-Boas mara baada ya Jana kunyukwa Bao 5-0 na Liverpool.
Kipigo hicho
cha ndio kimekuwa kisago kikubwa kwa Timu hiyo kwa Miaka 16 Uwanjani kwao White
Hart Lane na kimewaacha wakiwa Nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu England wakiwa
Pointi 8 nyuma ya Vinara Arsenal.
Villas-Boas,
Miaka 36, aliteuliwa Meneja Tottenham Julai 2012.
Mwezi Machi
2012, Villas-Boas alifukuzwa kazi Chelsea baada ya kuwa hapo kwa Miezi minane
tu.
Tottenham
ilipigwa Bao 6-0 na Man City hapo Novemba 24 na, ingawa walitoka Droo na
Mabingwa Man United na kuzifunga Fulham na Sunderland, kipigo hiki cha
Liverpool kimewachukiza Wamiliki wa Klabu hiyo ambayo mwanzoni mwa Msimu
ilimuuza Gareth Bale kwa Dau la Pauni Milioni 85 kwa Real Madrid, ikiwa ni
Rekodi ya Dunia, na kununua msululu wa Wachezaji ambao ni Paulinho, Roberto
Soldado, Nacer Chadli, Etienne Capoue, Christian Eriksen, Vlad Chiriches na
Erik Lamela lakini Timu imekuwa ikifanya vibaya kwenye Ligi.
Hata hivyo,
kwenye michuano ya Ulaya ya EUROPA LIGI, Tottenham imekuwa ikifanya vyema na
kushinda Mechi zao zote 6 za Kundi lake na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32
ambako leo wamepangiwa kucheza na Dnipro, Klabu ya Ukraine.
Mbali ya
mafanikio hayo, Villas-Boas pia ameipeleka Tottenham kwenye Robo Fainali ya
Capital One Cup ambako Desemba 8 watacheza na West Ham.
Villas- Boas
anakuwa Meneja wa 5 Msimu huu kutimuliwa kazi toka Klabu ya Ligi Kuu England
wengine wakiwa Steve Clarke, aliefukuzwa Jana kutoka West Bromwich Albion,
pamoja na Paolo Di Canio aliefukuzwa Sunderland Mwezi Septemba, Ian Holloway
alitimuliwa Crystal Palace Mwezi Oktoba na Martin Jol aliepoteza kazi
Fulham Wiki 2 zilizopita.
No comments:
Post a Comment