Rais wa
serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amekabidhiwa pia rasmu
hiyo na kueleza kuwa kuwa wajumbe watakaoteuliwa katika bunge la katiba
wanapswa kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa kamati hii iliyomaliza kazi
yake
Jaji mstaafu
Warioba amesema rasimu hii wanayoiwasilisha ni ndefu kuliko ile ya awali
iliyokuwa na ibara 240 wakati hii ina ibara 271 ikiwa ni matokeo ya tume
kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba yaliyotoa maoni mengine mapya.
Ameyataja
baadhi ya mambo ambayo tume imebaini kuwa yalijadiliwa kwa hisia kali katika
rasmu hiyo na ile ya awali kuwa ni suala la muungano hasa kuhusu muundo wake.
Amesema wakati tume inazindua rasmi ya awali hawakupendekeza kuendelea kuwa na
muundo wa serikali mbili ulihitaji ukarabati mkubwa ambao tume ilifikiri
hautawezekana, hivyo mabaraza ya katiba yalitoa mapendekezo mengi yaliyoilazimu
tume kufanya uchambuzi wa kina na kwamba iliwachukua muda mrefu wa tume.
Jaji Warioba
amesema wananchi Zaidi ya 39,000 wa Tanzania bara waliotoa maoni yao kuhusu
muungano na kati yao karibu 27,000 walizungumzia muundo na Zanzibar wananchi
karibia wote waliotoa maoni walijikita katika muungano ambapo kati ya wananchi
38,000 wa Zanzibar waliotoa maoni 19,000 walizungumzia muundo wa muungano.
Tanzania
bara asilimia 13 walitaka serikali moja, asilimia 24 walipendekeza serikali
mbili na 61 walipendekeza serikali tatu, wakati Zanzibar asilimia 34
walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 muungano wa mkataba ambapo asilimia
0.1 walihitaji serikali moja.
Hata hivyo
Rasimu hiyo ya katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeorodhesha malalamiko
10 kwa upande wa Zanzibar na manane ya Tanzania Bara.
Malalamiko
matatu makubwa kwa Zanzibar ni Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la serikali ya
muungano hivyo kupunguza nguvu kwa Zanzibar,Ongezeko la mambo ya
Muungano,kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Tanzania
bara tume hiyo imeyataja malalamiko kuwa ni kuwa Zanzibar imekuwa nchi huru ,
ina bendera yake ya Taifa, ina serikali yake ina wimbo wake wa taifa na
imebadili katika yake ili itambulike kama nchi wakati Tanzania bara imepoteza
utambulisho wake, wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi
Zanzibar wakati wenzao wanamiliki Tanzania bara.
ZAIDI SOMA HAPA:-http://www.scribd.com/fullscreen/194570319?access_key=key-useg6ebddqt21eummrr&allow_share=false&escape=false&show_recommendations=false&view_mode=scroll
No comments:
Post a Comment