![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP)
mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni
ya leo (Desemba 31,2013).
|
![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu
Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika
viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.
|
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua
Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014,
Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai
(Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua
Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi,
ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa
Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).
Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne,
Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
30 Desemba, 2013.
No comments:
Post a Comment