![]() |
Baadhi ya
Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar
wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.
|
Nyumba moja
iliyopo Mtaa wa Ugombolwa Kata ya Segerea jijini Dar imeteketea kwa moto mara
baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya
kimapenzi na mwanaume mwingine.
Hali hiyo
imetokea usiku wa kuamkia leo katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya
ya Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua
uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na
mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi
huo wa kuitia moto nyumba hiyo.
Mmoja wa
shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana, ebu ona
sasa mwanaume mzima anateketeza nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya
shilingi kisa mkewe anatembea nje ya ndoa.
Sasa watoto wake wataishi wapi?..
watu wengine ni wajinga sana, kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe
talaka tu" alisikika akiongea shuhuda huyo.
Mpaka mtoa
habari hii anaondoka eneo la tukio, nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea kwa
moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwa ajili ya
kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa
kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au lah huku ikikadiriwa
kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto.
Source:- JF
No comments:
Post a Comment