Miss Ngara 2013/2014:-Ni Usiku wa Desemba 31 ukumbi wa New Happy mjini Ngara na Hawa ndio washiriki,Nani kuibuka Mkali wao..??. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 25, 2013

Miss Ngara 2013/2014:-Ni Usiku wa Desemba 31 ukumbi wa New Happy mjini Ngara na Hawa ndio washiriki,Nani kuibuka Mkali wao..??.


Pichani ni baadhi Warembo ambao wamejitokeza kuwania Shindano la kumsaka Mrembo wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera :-Miss Ngara 2013/2014)  wakiwa katika Mapozi ya aina mbalimbali  wakati wa mazoezi ya Pamoja.


Warembo wanaojiandaa kuwania nafasi hiyo ni 10 ambao wamejitokeza mpaka sasa kwa Mujibu wa mhamasishaji wake Godwin Buchard (G2B) chini ya ufadhili wa Paradise Hotel  na Happy Fassion za mjini Ngara ambapo Shindano hilo linataraji kufanyika  usiku wa kuamkia Desemba 31,2013 katika ukumbi wa NEW HAPPY na lina lengo la  kuinua vipaji mkoani wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Katika Shindano hilo ,Mshindi wa  kwanza ataondoka na  Vifaa vya saloon ya kike vyenye thamani ya shilingi Milioni 2,Mshindi wa pili atapata Jokofu  lenye thamani ya shilingi Laki 7 na watatu zawadi yake ni cherehani yenye thamani ya shilingi Lakini 5.



Akizungumza na Mwana wa Makonda Blog Mmoja wa waratibu wa Miss Ngara 2013/2014-Godwin Buchard( G2B) amesema washiriki wote wanataraji kuingia kambini kuanzia wiki hii(Desemba 26,2013) na wakiwa kambini ,pamoja na mambo mengine Watajifunza mbinu za kupambana na VVU/UKIMWI,kupambana na Rushwa,Madawa ya Kulevya ,Ujasiriamali,Namna ya kutunza na kuhifadhi mazingira ,Elimu ya Uzazi pamoja na Kutoa misaada mbalimbali kwa makundi yenye uhitaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad