Klabu ya
Manchester United imetoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2 dhidi ya Hull
City katika Uwanja wa KC, huku James Chester, Mchezaji alieanzia Soka lake huko
Old Trafford, ameifanya Man United ishinde mchezo huo baada ya kujifunga
mwenyewe Bao la 3 katika Dakika ya 66.
Chester ndie
alieipa Hull Bao la kuongoza na ndani ya Dakika 13 waliongoza Bao 2-0 baada ya
Shuti hafifu la David Meyler kumbabatiza Jonny Evans na kumhadaa Kipa De Gea.
Lakini Man
United walizinduka na Chris Smalling kuunganisha kwa kichwa frikiki nzuri ya
Wayne Rooney na kufunga Goli la Kwanza na Dakika 7 baadae Wayne Rooney
aliisawazishia Man United kwa Bao tamu baada kusogezewa na Danny Welbeck.
Hilo ni Bao
la 150 kwa Rooney kwenye Mechi za Ligi akiwa na Man United na kumfanya awe
Mechezaji wa Pili kufikisha idadi hiyo akichezea Klabu moja tu na mwingine ni
Thiierry Henry aliekuwa Arsenal na kufunga Bao 175.
Hadi
Haftaimu Bao zilikuwa 2-2 na ndipo Kipindi cha Pili Chester alipojifunga kwa
kichwa baada kuicheza krosi ya Ashley Young iliyokuwa ikielekea kwa Rooney.
Valencia
alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Dakika ya 90 baada kupewa Kadi ya Njano
ya Pili kwa kupoteza muda kwa makusudi.
|
No comments:
Post a Comment