![]() |
Wadadisi wa
Soka wanasema ikiwa Manchester United itaendelea kushindwa michezo yake ya Ligi
kuu Uingereza (EPL)huenda isiwe katika nafasi za kwanza hadi nne katika Msimamo
wa Ligi.
|
Manchester
United Jumamosi (Desemba 07,2013) lipata kipigo chake cha pili nyumbani katika
muda wa siku nne baada ya kulazwa bao moja bila na New Castle.
Mchezaji wa
New Castle Yohan Cabaye ndiye aliipatia kilio Manchester United huku kwao ikiwa
kicheko baada ya kushinda Manchester United kwa mara ya kwanza nyumbani Old
Trafford tangu mwaka 1972.
Man United walikuwa na wakati mgumu kuvunja ari ya
Magpies na kukosa nafasi kadhaa za mabao mfano Patrice Evra alipogonga lango
huku mpira ukirudi na kumgonga mkono Vurnon Anita.
Mpira wa
kichwa wa Robin van Persie haukuzaa matunda kwa Manchester United,lakini
Newcastle waliishia na kicheko baada ya kupata ushindi wao wa kihistoria dhidi
ya Man United.
Bila shaka
hii inazua wasiwasi mkubwa kwa David Moyes kwani Man U wanaendelea tu kudidimia
kwa mabao.
Man United wameshuka ngazi hasa baada ya kupata kipigo
mara mbili mfululizo tena nyumbani Old Trafford ikiwa ni mara ya kwanza kwa
hali hii kushuhUdiwa kwa United.
Mnamo
Jumatano walilazwa na Everton huku wakiwa nyuma ya Arsenal kwa pointi 12
wakikabiliwa na tisho la kutokuwa katika msitari wa mbele kuwania kombe la ligi
ya Premier.
Ikiwa
wataendelea kushindwa hivi Man U hata huenda wasiwe katika nafasi za kwanza
hadi nne katika msimamo wa Ligi.
![]() |
Oussama
Assaidi scored a superb late winner as Stoke City came from behind to stun
Chelsea and earn just their fourth Premier League win this season.
|
Manchester United 0-1 Newcastle
Southampton 1 – 1 Manchester City,
Liverpool 4 – 1 West Ham United,
Stoke City 3 – 2 Chelsea
West Brom 0 - 2 Norwich
Palace 2 – 0 Cardiff
1 | Arsenal | 14 | 19 | 34 |
2 | Liverpool | 15 | 16 | 30 |
3 | Chelsea | 15 | 13 | 30 |
4 | Man City | 15 | 26 | 29 |
5 | Everton | 14 | 9 | 27 |
6 | Newcastle | 15 | -1 | 26 |
7 | Tottenham | 15 | -2 | 25 |
8 | Southampton | 15 | 5 | 23 |
9 | Man Utd | 15 | 3 | 22 |
10 | Aston Villa | 14 | 0 | 19 |
11 | Swansea | 14 | 1 | 18 |
12 | Stoke | 15 | -5 | 17 |
13 | Hull | 14 | -6 | 17 |
14 | Norwich | 15 | -14 | 17 |
15 | West Brom | 15 | -4 | 15 |
16 | Cardiff | 15 | -11 | 14 |
17 | West Ham | 15 | -6 | 13 |
18 | Crystal Palace | 15 | -12 | 13 |
19 | Fulham | 14 | -14 | 10 |
20 | Sunderland | 15 | -17 | 9 |
No comments:
Post a Comment