Kilimanjaro Stars wametinga Nusu Fainali ya CHALENJI CUP baada ya kuwatupa nje Mabingwa Watetezi Uganda kwa Penati 3-2 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 07, 2013

Kilimanjaro Stars wametinga Nusu Fainali ya CHALENJI CUP baada ya kuwatupa nje Mabingwa Watetezi Uganda kwa Penati 3-2 .

 Kipa  Ivo Mapunda leo (Desemba 07,2013) ameibuka shujaa baada ya kuokoa penalti mbili za Dani Sserunkuma na Khalid Aucho wa Uganda na kuipa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ushindi wa penalti 3-2 baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya.

Wachezaji wa Stars wakimbeba Kipa wa Kilimanjaro Stars, Ivo Mapunda baada ya kuokoa penaltri ya Dani Sserunkuma wa Uganda.


Mbali na kuokoa penalti hizo mbili, Uganda walipoteza penalti nyingine moja baada ya Godfrey Walusimbi kupiga, wakati Hamisi Kiiza Emannuel Okwi ndiyo pekee walioifungia Cranes penalti.

Penati za Kili Stars zilifungwa na Kevin Yondan, Athumani ‘Chuji’na Erasto Nyoni huku Samatta na Kiemba wakipoteza Penati zao.


JE WAJUA?

- Uganda wametwaa Chalenji Cup mara 13 na Tanzania Bara mara 3.

- Uganda waliitoa Kilimanjaro Stars 3-0 kwenye Nusu Fainali Mwaka Jana.

- Mara zote 3 Tanzania Bara ilipotwaa Chalenji Cup imekuwa ikiifunga Uganda. 
Mwaka 
1974 waliitoa kwa Penati 5-3 baada Sare ya 1-1, 1994 waliifunga 4-3 kwa Penati baada Sare ya 2-2 na Mwaka 2010 kwa Penati 3-2 baada Sare ya 0-0.



Katika Mechi hiyo, Uganda walitangulia kufunga katika Dakika ya kwa Bao la Sserunkuma lakini Mrisho Ngassa, akipokea pande toka Mbwana Samatta, alisawazisha katika Dakika ya 21 na Ngassa tena kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 38 kwa frikiki baada Samatta kuchezewa Rafu.

Refa Wish Yabarow wa Somalia aliipa pigo Kilimanjaro Stars katika Dakika ya 53 kwa kumtoa kwa Kadi Nyekundu Kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Katika Dakika ya 73, Uganda walisawazisha baada ya Kona iliyomkuta Martin Mpuga na kufunga.
 
Mshambuliaji wa Kenya, Haambee Stars, Jacob Keli akiwatoka mabeki wa Rwanda, AmavubiBayisenge Emery kulia na Tubane James kushoto Uwanja wa Manispaa, Mombasa leo(Desemba 07,2013).
Sasa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itamenyana na wenyeji, Kenya, Harambee Stars katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Desemba 10, mwaka huu Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

Hiyo inafuatia Kenya kuifunga Rwanda 1-0 katika Robo Fainali ya pili CECAFA Challenge jioni hii Uwanja wa Manispaa, Mombasa Kenya, bao pekee la beki wa Azam FC ya Dar es Salaam, Joackins Atudo kwa penalti dakika ya 56.

Mapema katika Robo Fainali ya kwanza, Stars iliwatoa mabingwa watetezi, Uganda kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.

Robo Fainali nyingine zitachezwa kesho(Desemba 08,2013), Ethiopia na Sudan na Zambia na Burundi, Uwanja wa Manispaa pia.


RATIBA/MATOKEO 2013/2014.

SIKU
NA
ROBO FAINALI
MJI
SAA
Jumamosi Desemba 7
19
Uganda 2 Kili Stars 2 -Stars wasonga Penati 3-2
Mombasa
1400

20
Kenya v Rwanda
Mombasa
1600
Jumapili Desemba 8
21
Zambia v Burundi
Mombasa
1400

22
Ethiopia v Sudan
Mombasa
1600

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad